Hivi nchi hii nani katuloga na hizi mindset za kijinga kiasi hiki? Kuwa kingereza kizuri ndo kipimo Cha elimu bora ni kweli??!
Hivi mtu aliyesoma English hapo kwa Ras Simba utamweka kwenye level moja na Ndalichako in terms of intellectual content hata Kama anatiririka English vizuri kuliko Ndalichako?! Mfano Harmonize umlinganishe na Ndalichako.
Mnatakiwa muelewe kitu kimoja kuwa Elimu ni kiwango cha maarifa alichonacho mtu kichwani na siyo uwezo wa kumudu Lugha fulani kwa ufasaha. Lugha inatusaidia kuwasiliana tu, na kiwango cha English ya Ndalichako kinamtosha kabisa kuweza kutumia maarifa yake katika kazi zake.
Hivi hushangai huyo unayemsema amekuwa katibu mtendaji wa baraza la mitihani kwa muda mrefu tu, bila shaka hata cheti chako kina sahihi yake, amefundisha Udsm kwa miaka kadhaa, unafikiri katika kutekeleza majukumu hayo hakutumia English?!!
Sent from my itel W6004 using
JamiiForums mobile app