Rais Samia: Kijana aliyeongoza Uokoaji atafutiwe nafasi Jeshi la uokozi

Rais Samia: Kijana aliyeongoza Uokoaji atafutiwe nafasi Jeshi la uokozi

Safi sana,hongera zake

Lakini ukiangalia upande wa pili kama sio haraka zake inawezekana hyo ndege ingevutwa mpaka kwenye kina kifupi na ndo mlango ungefunguliwa wangeweza kutoka watu wengi zaidi,labda hata vifo visingekuwepo,maana baada ya kufunguo huo mlango maji yalianza kuingia ndani ya ndege
 
Asante kwa serikali kuliangalia hili lakini pamoja na offer hiyo waangalie pia huhitaji wake? inawezekana ni Engineer au mwanasheria au Mhasibu lakini kutokana na mazingira ya kukosa ajira ikabidi aingie kwenye uvuvi.
hivyo ikitokea anafani zaidi na angependa apate alichosomea ni bora wafikirie hivyo.
vinginevyo kama Wazungu sio wabinafsi anastahili kuingizwa kwenye guinness book records 2022 na kupokea zawadi inayoendana na yeye jina la tuzo hiyo.
MWENYEZI MUNGU akutunze
 
Itategemea na utayari wake. Najua ajira ya ziwani inalipa kuliko kuajiriwa serikalini.
Itapendeza kama angewezeshwa zana muhimu za kazi yake ili ajiendeleze zaidi.

Kama elimu hajaenda sana atapewa laki tano kwa mwezi na hakuna marupurupu.

Itamfanya arudi ziwani tena
 
Hata akiwa Hana cheti wamfadhili asome QT apate ajira,
SI hii biashara ya wenye ajira na marupurupu kibao wakisisitiza watu wajiajiri kama ni kitu kirahisi vile!!
QT ili apate likaratasi la cheti? Waachane na makaratasi ya vyeti huyu ni mtendaji, afanyiwe training kwa vitendo aingie mzigoni.
 
Mama amefanya vzr zaidi. Huo ndo ushujaa unaotakiwa. Na amepewa kile ambacho anastaili. Nataman waanzishe bakuli la kumpongeza angechukua 100k yangu bila kinyongo. Nina imani hata manusula lazima watamtafuta badae wamtoekiushikaji. Dogo kapata umaarufu wa hatari
 
Ni agizo kutoka kwa Rais Samia

Amiri Jeshi Mkuu ameagiza Waziri wa mambo ya Ndani mh Masauni kuanza mchakato wa ajirar ya huyo kijana mara moja

Kijana huyu ndio alizamia na kwenda kufungua mlango wa ndege na hatimaye abiria 24 wa Precision Air iliyozama kuokolewa

Source TBC

======

Waziri mkuu akiwa kwenye shughuli ya kuaga miili ya kuaga marehemu waliopata ajali kwenye ndege ya precision amesema Rais Samia ametoa agizo kijana aliyewanusuru watu waliokwama kwenye ndege hiyo atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la uokozi.

Pia Serikali kugharamia mazishi ya wote waliofariki kwenye ajali hiyo.
Cha ajabu pamoja na kujua kwake kuogelewa kikiwa kama kigezo kilichomuwezesha kuogelewa, akimaliza mafunzo utasikia kapangiwa zimanoto singida au dodoma
 
Safi sana,hongera zake

Lakini ukiangalia upande wa pili kama sio haraka zake inawezekana hyo ndege ingevutwa mpaka kwenye kina kifupi na ndo mlango ungefunguliwa wangeweza kutoka watu wengi zaidi,labda hata vifo visingekuwepo,maana baada ya kufunguo huo mlango maji yalianza kuingia ndani ya ndege
Wewe ulikuwa ndani ya ndege ama unaandika tu nyuma ya keyboard?
 
Mkuu, suala hapo ni Rais ameguswa na uhodari, ujasiri na uthubutu wa kijana iliyopelekea Watanzania wenzetu kunusilika kufa majini. Jambo hili limepelekea kuagiza apewe kazi yenye kuendana na kazi nzuri aliyoifanya.

Ukiondoa pengine suala la yeye kuwa mfariji kwa wafiwa na majeruhi wa ajali, hayo mengine sijui mwenye huruma, sijui ni mwenye kujali n.k. sidhani kama ulipaswa kuyagusia hapa katika hoja iliyopo mezani.
Yote niliyoyaeleza Ni Tabia njema za kizalendo alizonazo Rais wetu
 
Yote niliyoyaeleza Ni Tabia njema za kizalendo alizonazo Rais wetu
Ndiyo! Lakini mkuu maoni kama hayo uliyoyatoa yalipaswa kuwekwa kwenye uzi wenye maudhui kama hayo. Lakini katika uzi huu ilitosha tu ujikite katika kutambualiwa kwa uhodari wa kijana jasiri mbele ya Rais na hatimaye akaambulia cheo, jambo ambalo litachochea hamasa ya vijana wengi kujitokeza pindi changamoto zitapoijitokeza.
 
Rais Samia suluhu hassan ameagiza kijana aliyewaokoa watu 24 kwenye ajali ya ndege ya bukoba jana atafutiwe kazi kwenye jeshi la uokozi

"Tukiwa hapa kwa RC anaongea na kutoa shukrani za pongezi,Rais ametupigia simu hapa na kutuagiza Akabidhiwe kwa Waziri wa mambo ya ndani,nae pia atafutiwe nafasi kwenye jeshi la uokozi ili kijana huyu apewe mafunzo zaidi,kwa ujasiri wake huo aingie kwenye jeshi hilo ambalo linahitaji ujasiri aliouonesha---amesema waziri mkuu Kasim Majaliwa
Credit: Millard Ayo
 

Attachments

  • Screenshot_20221107-143747~2.png
    Screenshot_20221107-143747~2.png
    101.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom