Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ahh kweli we ni chawa... Ni ziara ndefu na itatugharimu sana. Lakini yaweza kuwa na mafanikio. 🥳🥳🥳
 
Ni ziara yenye manufaa makubwa sana kwa Taifa letu.kwanza angalia tu hapo mapesa tutakayo yapata tena kwa masharti nafuu kabisa. Hapo bado makubaliano na mashirikiano katika Secta mbalimbali yatafanyika na kusainiwa.kwa ufupi ni ziara moja yenye tija kubwa sana kwa Taifa letu na maendeleo ya Taifa letu.
 
ZIARA NZITOYA KIKAZI KWA MUDA WA WIKI MOJA🤣🤣

Bonge la Movie la Kikorea litegemewe muda wowote hapo.
Kumbuka pia kuwa kuanzia tarehe 4-6 June kutakuwa na mkutano utakao wakutanisha wakuu wa nchi na serikali kutoka Afrika kwa upande mmoja pamoja na Korea ta kusini ,Ambapo katika mkutano huo Rais Samia atatoa hotuba nzito sana.
 
Screenshot_2023-01-08-12-31-48-671_com_1697943223785.pinterest.jpg
 
Kumbuka pia kuwa kuanzia tarehe 4-6 June kutakuwa na mkutano utakao wakutanisha wakuu wa nchi na serikali kutoka Afrika kwa upande mmoja pamoja na Korea ta kusini ,Ambapo katika mkutano huo Rais Samia atatoa hotuba nzito sana.
Nzito sana, kilo 150 siyo
 
🔨🔨🔨🔨👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C7jsRsUoNTf/?igsh=NWUxb3VwN2pycnh2
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ahsante kwa Taarifa Zuhura Yunusu
 
Back
Top Bottom