"Kutokana na Mkoa wetu kuendelea kurejea katika hali yake ya amani Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atazungumza na wazee wa Dar es Salaam kesho tarehe 2 disemba, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC kuanzia saa tano asubuhi.
Katika kuzungumza na wazee wa Dar Es Salaam atatumia nafasi hiyo kuhutubia taifa.
View attachment 3509899
Nitoe rai kwa wana-Dar Es Salaam na Watanzania kumsikiliza Mhe. Rais atakapokua anazungumza na wazee wa Dar Es Salaam""Ni moja ya hatua kubwa anayochukua kuhakikisha nchi yetu inarejea katika amani katika kuhutubia huko ataambataana na viongozi wengi wasio wa serikali pamoja na viongozi wasio watumishi wa umma ni mkutano muafaka na kuendelea kuponya pale ambapo watanzania waliumia."
Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert John Chalamila wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 01, 2025.