Rais Samia: Kuna mtu kakopa benki zetu 5 katoweka

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.

“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”

“Kuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?

Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”

WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?

Atakuwa kama Fataki kupata umaarufu kwa kutajwa na ngazi za juu
 
Nilichokuja kugundua

Tanzania inahitaji mtu mtukutu kutuongoza km mzee baba asee
Mzee baba mwenyewe ripoti kama hizi aliziogopa sana tu rejea kutenguliwa kwa prof Assad, watanzania tunatabia za kinafiki sana si ajap kuona tunamtukuza rais kuliko taifa lenyewe. Rais sio Mungu wala Malaika Kuna muda na wakati anaitaji msaada kisayansi, kimedani na ujuzi kuweza kukabiliana na uvujaji wa mapato ya nchi.
 
.........rais Samia kwa sasa anafahanu mengi kuhusu uongozi wa nchi serikali na watendaji Kwa ujumla lakini yeye ni mtu mwenye subira na mvumilivu sana..... ndo maana watu wanaona kama mambo yanaharibika au hachukui hatua, hii sio kweli huyu mama ni menda haki.......na niseme tu zinakuja siku ambazo mama atachukua hatua kali sana Kwa baadhi ya watendaji na watu hawataamini........ni swala la muda tu......
 
Hotuba ya leo imeonesha ameanza kupata uhalisia! Nafikiri hadi mwaka wa tatu ramani zote zitakuwa mkononi! Sometimes ukiwa mgeni wa mambo unaweza kufikiri wenzako walikuwa wazembe kumbe wazee walitulia uone mwenyewe kabla dossier hazijaanza kuachiwa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom