Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nchi inakatisha tama sana, viongozi wanalalamika tu hawawezi kuchukua hatua wala maamuziHata mimi ningekua na access hiyo ningekopa na kutokomea kusikojulikana
Kama hakuna mtu wa kuwawajibisha wezi tusilalamike.
Na hapo ndipo simuelewagi samia, kama Rais nae analalamika sisi tufanyaje ? Wakati maamuzi yote yapo mikononi mwake.Sasa kama rais naye anaishia kunung'unika inakuwaje?
Ndio imeisha hiyo, wizi mkubwa wote unaanzia serikalini..........rais Samia kwa sasa anafahanu mengi kuhusu uongozi wa nchi serikali na watendaji Kwa ujumla lakini yeye ni mtu mwenye subira na mvumilivu sana..... ndo maana watu wanaona kama mambo yanaharibika au hachukui hatua, hii sio kweli huyu mama ni menda haki.......na niseme tu zinakuja siku ambazo mama atachukua hatua kali sana Kwa baadhi ya watendaji na watu hawataamini........ni swala la muda tu......
Kwanza nashangaa rais analalamika badala ya kuwachukulia hatua, kwanza hapo anapoongea alitakiwa kuwaagiza polisi kuwashughulikia wahusika kuanzia muda huo.Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.
“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”
“Kuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?
Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”
WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?
Endelea Kutupa Nukuu ya Hadithi uliyo Simuliwa na Babu yakoRais mwenye akili timamu na mzalendo
Tanzania ni nchi rahisi sana kuipiga hela ukiwa smart kichwani yaani hutumii nguvu sana.. Huyo mfanyabiashara ametisha..Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.
“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”
“Kuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?
Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”
WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?
Mzee baba mwenyewe ripoti kama hizi aliziogopa sana tu rejea kutenguliwa kwa prof Assad, watanzania tunatabia za kinafiki sana si ajap kuona tunamtukuza rais kuliko taifa lenyewe. Rais sio Mungu wala Malaika Kuna muda na wakati anaitaji msaada kisayansi, kimedani na ujuzi kuweza kukabiliana na uvujaji wa mapato ya nchi.
Kinarudishwa kile cha "miaka 6"Hili nalo mkaliangalieni vizuri.
Haya mambo sio ya kufumbia macho Wala kutamka kimafumbo. Kama Benki zipo waliohusika ni watumishi, sahihi zipo, pesa zikiingizwa akaunti gani na ya jina la nani kwenye Benki gani mahali gani? Na zilihamishwaje Kuna haja gani kuogopa kuwapatia wahusika?
Au ndio Shamba la bibi linazidi kupakuliwa?
MaChawa mpo?!