Rais Samia: Kuna mtu kakopa benki zetu 5 katoweka

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.

β€œKuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”

β€œKuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?

Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”

WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?

Huyu ni rais anayeongoza nchi?

God have mercy on us.
 
Kila mtu analalamika, nani wakuchukua hatua sasa.

Hapo amri ni moja tu, kamata wote tupa ndani, uhujumu uchumi na money laundering mahabusu 20yrs, hukumu 100yrs. Na mali zote mali ya serikali.

Ukifanya hivi x 10 tu kila mtu ataogopa mali ya umma..

JPM alikomaa na wale matycoon wa Unga wakalambwa mvua za kutosha, kuanzia wauza mirungi, bhangi na unga woote ukijaa nyavuni unakula mvua wote wakaiogopa dola...Sasa hivi imeshakuwa oya oya wauza powder wameanza tena kutamba.
Tatizo Sasa hivi Ni kwamba, atatumwa Nani akamkamate Nani?
Waziri wanajua alivyoiba
Karibu mkuu mwizi
Makamishna wezi
Wakurugenzi wezi
Takukuru imekua rukukuta
Polisi imekua polisi jazz bend
iPhone inanunulika kiulaiiini.
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.

β€œKuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”

β€œKuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?

Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”

WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?

Acha utani.
Dunia hii ya leo kuna "mtu kutokomea kusikojulikana"?
 
Hahahahahaaa.. tatizo lingine unakuta pengine, watu hao wanaoiba ndo wanakuja fadhili Chama au serikali kupitia mlango wa uwani.....kaazi kweli kweli..
We kufadhili wapi pesa zinasombwa ulaya watu wana invest kwenye ma bonds, real estate, bitcoin na asset zingine kipindi cha Kikwete kuna waziri siwezi mtaja alisepa na 66B ana 5 star hotel 3 nchini Canada hivi vitu mkuuu havinaga muongozo asee

Watu wanajali vizazi vyao tu hapa
 
Rais Samia amesema kuna ushirikiano wa wanaoenda kukopa na maafisa wa benki na wahusika wapo lakini wanatizamwa tu na wanajua walichokifanya
Sasa anamwambia nani?. Tuna kiongozi dhaifu sana, majizi yapo kila kona yeye asichukue hatua aendelee kuwabembeleza aone atakachovuna. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom