Kwanza anasema.. watu wanazunguka na anawatizama! 😂 hapo mkuu unadhani kitafanyika kitu gani?
Kuwashauri CCM ni matumizi mabaya ya muda, kwenye mabo ya ufisadi, wote wanashirikiana vizuuuri sana, ila tu wanachokifanya, watahakikisha mmoja wao anakuwa mpiga kelele kana kwamba jambo halijui, kumbe usiku wanakuwa wote
Lingine! Tanzania tutapitia shida nyingi sana kiasi cha wengine kubakia godoro za kulalwa tu wengine huku wao wakiwa na kila kitu, godoro ndo linabaki na maumivu ya wanaolilalia
Inakuweje hata watoto wa viongozi wakuu wa vyama pinzani mbakimbali wabapelekwa nje kusomeshwa na serikali?
Hao watu watakuwa na uchungu na Watanzania walala hoi kweli
Wanaroho ya kupigania wasiojiweza nchini kweli?
vyama vyote vinajuana saafi kabisa, wate lao moja!
Mmawia ndugu yangu, najua unapenda sana upinzani kama ilivyo kwa wengi, lakini, wana mambo mengi sana ya kuwatilia mashaka iwapo kweli wana udhati wa mioyo yao kuikomboa Tanzania kutoka kwenye makucha ya ccm kinacho wala wananchi
Tufanyeje sasa?