Nimewiwa na Furaha na nashindwa Kuelezea jinsi nilivyopokea Taarifa kuwa Kesho Rais wa Tanzania Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia Kuanza Ziara ya Siku Mbili nchini Rwanda kwa Mwaliko wa Mwenyeji wake Rais Paul Kagame.
Rais Samia asikudanganye Mtu Mama yangu kama kuna Marais ambao wanaipenda na Kuiheshimu Tanzania na wanawapenda Watanzania ndani ya Mioyo yao kabisa basi ni Mzee Yoweri Museveni na huyu Paul Kagame unayeenda Kukutana nae Kesho.
Upendo wa Marais Kenyatta wa Kenya na Ndayishimiye wa Burundi kwa Tanzania ni wa 'Kinafiki' na 'Maslahi' zaidi ila Upendo wa Waganda ( Museveni ) na Wanyarwanda ( Kagame ) kwa Watanzania ni wa kutoka Rohoni na Moyoni kabisa.
Najua Tanzania ni 'Millitary and Intelligence Giant' kwa Ukanda Wetu huu wa Maziwa Makuu, ila kwa Uweledi na Umahiri wa Masuala ya Kijeshi, Kiusalama, Kibiashara, Kimkakati, Ubunifu, Teknolojia na Kimahusiano alionao Rais wa Rwanda Paul Kagame najua yapo ambayo utafaidika nayo Kwake na Yeye pia kuna Mema ya kutoka Kwako ( Tanzania ) atafaidika nayo ili basi kwa pamoja Tanzania na Rwanda zipige hatua Kimaendeleo na kwa Ustawi wa Wananchi wake ( wao )
Tafadhali Rais Samia usisafiri kwenda Rwanda Kesho ukiwa umebeba Kichwani mwako yale Mawazo Potofu na ya Chuki kutoka kwa baadhi ya Watanzania wasiojielewa kuhusu nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wake ( wao ) Paul Kagame. Rwanda inaipenda Tanzania na Wanyarwanda wanawapenda mno Watanzania na tambua tunaingiliana pia hata 'Kindugu' vile vile.
Mimi kama GENTAMYCINE nakutakia Safari njema, Mapokezi mema, Ziara njema, uifurahie Rwanda na urejee salama kabisa nchini Tanzania ili uyafanyie Kazi yale mema utakayokutana nayo huko na uyatumie pia katika Uongozi ( Utawala ) wako hapa nchini Tanzania.