Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.



===

Rais Samia: Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge”

Rais Samia: “Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na Watoto wako na Mama Watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue Mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, Nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu

Na yeye aache chokochoko
 
Hawa wanajifanya wehu hawa.

Dawa yao ni kwenda nao hivyo hivyo kiwehu wehu.

Yaani mama aache kushughulikia Watanzania wote wapate umeme aanze kushughulikia matakwa yao wao. Ikifika 2025 waanze kumuuliza mbona umeme hakuna????

Tutakwenda nao wanavyotaka wao
Tena yaliyomo kwenye ilani ndiyo yaliyotufanya sisi tukaichagua CCM. Tumeshamkumbusha Mama kwamba hatukukichagua chama chake ili kianze mambo yasiyo ya msingi. Tumekichagua ili kitekeleze waliyotuahidi kupitia ilani.

Ni imani yetu kuwa imani itatekelezwa na hizi kelele za hawa wahuni zitapuuzwa
Makamanda wanataka wampangie ratiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa kiongozi huwezi kumridhisha kila mtu au kila kundi
ukitaka kumridhisha kila mtu au kila kundi unaweza kukumbwa na mambo makubwa mawili:
1. utachelewa sana kufikia malengo.
2. Unaweza kupoteza mwelekeo.

Kinacho takiwa ni kufanya maendeleo yanayo wagusa wananchi wengi.
Madai ya katiba mpya ni madai ya kikundi kidogo cha wanasiasa wachache.
wananchi walio wengi mijini na vijijini wanataka kasi ya maendeleo iongeze, tunamuomba Rais wetu asicheleweshwe na kelele za watu wachache, wananchi wengi ambao hawapigi kelele wanamatumaini makubwa na yeye.
Kanyaga twende mbele kwa mbele.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio rahisi kama unavyosema mzee mzima

Hapa ni watu milioni 60 wanawaangalia mnavyotoa majibu ya kipumbavu...

Mtakataa ndio,kwa hoja gani yenye mashiko watu milioni 60 wawaelewe?

Hakuna majibu sahihi,mmeishia mipasho

Katiba Mpya ni muiba ambao hamkumaliziaga sababu ya matamaa yenu ya kutaka iwe ya kiCCM,sasa huu muiba umerudi kuwachoma

Raha ya tatizo ni kulifanyia suluhisho tena mapema..

Watch this space...
Watu milioni 60 ndio wanadai katiba?

Mbona naona ni kakikundi kadogo tu huko twiter
 
Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki,wananchi tulipiga kura na CCM ikashinda.,nyie wengine kura hazikutosha.
Onyesha sehemu aliyosema wameiba kura..
Huu ndiyo unauita kuwa ni uchaguzi huru na haki?👇Umechanganyikiwa?
7654311.png
 
..hawahawa wapinzani tunaoambiwa ni WAOGA ndio wavunje amani ya Tanzania?

..na ukitaka kujua kuwa anaongea lakini hamaanishi anachokiongea ni matumizi yake ya neno " vijichokochoko. "

..that means there is nothing to worry about. Hakuna hatari yoyote ile.
Mama anaupiga mwingi sana [emoji847]
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mbowe kachaguliwa kwa kura zipi hapo ufipa? Mwenyekiti wa milele ndio apewe nchini si atakomalia madarakani kama mzee M7
Mbowe ndio alikuwa Raisi wa nchi kwa kuchaguliwa kwa kura ??? Umeshiba mbegeau Mbio Za mwenge zimekuchosha leo?
 
Swala la katiba lina umuhimu wake... Na sisi watz siku tukiacha unafiki ndo inchi itasonga mbele..... Ni juzi tu mlikuwa mkilia lia magu hafati sheria leo hamtaki tena katiba?? Binafsi naitaka katiba na sio kwasababu za chadema"" ila i wish katiba mpya iwepo na ifute mamlaka ya raisi kutowajibishwa pamoja na viongozi wa wakuu wa nchi!!!! Yani hili ndo linanikera kwamba raisi haguswi, spika wa bunge haguswi, jaji mkuu wa serikali haguswi, DPP haguswi... Hii katiba haifai yani inawaruhusu wao kufanya watakavyo kwasababu hawaguswi!!! Kwa mfano hii kauli ya mama haifai ukiwa mkuu wa nchi lazima uwe na solution yakumaliza tatizo na wapinzani wako sio kutisha raia kwamba wataumia.... Kwa kauli hii raisi kwenye nchi za wenzetu unashitakiwa ni kauli yakichochezi hupaswi kuongea kwenye hadhara ya watu!!! Mamlaka ya raisi lazima yawe na mipaka na katiba ile kwasababu inchi kama ichi hatuna vision kila raisi anakuja na lake' atavyojisikia yeye ndo atafanya sio kwa mujibu wa sheria yani afate sheria!!! Tuone kuna umuhimu wa katiba lengo sio chadema kutawala au kutaka madaraka... Ije katiba mpya hata kama CCM itaendelea kuongoza ila katiba iwepo na waifate ili wasipofata sheria katiba iyo iyo iwawajibishe... Lakini hii iliyopo naona kama kila kitu ni ndio na imewabeba viongozi wakuu na ndo sababu wanaropoka tu!!! Kwakauli ya jana ya mama ina tofauti gani na mdude akiropoka kwenye majukwaa ya Siasa???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja zipi amesema anajenga uchumi kwanza take it! Mambo ya katiba atayashughulikia kwa wakati maalumu. Hilo jibu hamlitaki sasa mnachotafuta nini kama si chokochoko? Mwendazake alisema kuna watu wanawashwa washwa!
Kumbe akiwashwa yeye, kaipata dawa katokomea kuzimu
 
Watu washaona Rais ni jinsia ya Kike basi ndio wanataka kujionesha kuwa wao ni vidume.
 
Back
Top Bottom