Rais Samia nakushauri watose sasa Spika (Tulia) na PM (Majaliwa), sakata la bandari limekumaliza kisiasa!

Wewe kasome ripoti ya Sekretariet ya bunge.., halafu kajibizane nao. Kwamba serikali ilikuwa inapinga nini kwamba si mkataba bali ni makubaliano?
Tatizo ni lugha tu. Nimekwambia kiswahili kina upungufu wa baadhi ya maneno.

Maana ni ile ile ya mkataba uliopita bungeni wa IGA. Unaweza pia kuliita azimio la makubaliano ya kufanya biashara pamoja kati ya Dubai na Tanzania.
 
Hizo ndoto zako zingewezekana ikiwa tu angekuwa amekwepa mtego wa kuanguka SAHIHI yake.
 
hahaha aaaa.umenichekesha .what if hao uliyowataja hawajahi kuwa consulted ? nao wafanyeje? nafikiri hamna haja ya kualaumiana.mkataba tuuache tujenge nchi yetu.maana kabla ya mkataba huu hakuna mwananchi aliyekufaa kwa njaa na hatutakufa kwa njaa.
 
Ina maana Hawa viongozi wawili wameingizwa chaka na watoto wa mjini???!
 
Mmh hili la bandari limetuvua nguo hadi sisi kina mama. Tumeonekana ni dhaifu, hatustahili kupata madaraka makubwa ya kiuongozi.
 
Spika ni mhimili mwingine kabisa na Raisi kimamlaka hana uwezo wa kumtoa spika, ni Tanzania tuu watu wanafikiri Raisi ana mamlaka juu ya bunge, tatizo la CCM na wabunge wake wameingia kwa wizi uliodhaminiwa na serikali ndio maana wabunge wote wamegeuka kuwa chawa tuu
 
Watu wengi waliokuwa wanamuona Rais Samia kama rais bora wa mfano, kwa sasa (kupitia suala la bandari) wanamuona Rais wangu kama mtu mwenye upeo mdogo au mwenye tamaa kubwa za kifisadi kuliko mwanasiasa yoyote aliyewahi kutokea hapa Tanzania. Sakata la bandari limeondoa heshima yote ya Rais Samia.[emoji2827][emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika,mama aliituluza nchi ,lakini hili la Bandari amelikoroga !
 
You nailed[emoji419][emoji419] it
 
Atawatosaje hao?
Kwani aliyesaini mkataba wa DP World ni Majaliwa au Spika?

Kwa kifupi hawezi kuwatoa sadaka wakati mkataba aliusaini yeye mwenyewe.
 
Hakuana namna nyingine waondoke kwenye ofisi za umma kumuondolea Rais aibu hii kubwa.
 
Serikali hiyo hiyo inayoongozwa na PM na Spika muda huu inajiandaa kusaini mikataba ya Consession na Lease, wewe endelea tu kuishi na mawazo yako mgando.
Nani kabisha juu ya hilo?

Hoja ni ile ile, kwamba huo ni mkataba na si makubaliano, maana yake uozo wote uliopo ndani ya huo mkataba una meno na ni ‘legally binding’.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…