Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Hakika.
 
Wamkumbushe kitabu kinachoitwa katiba ndiyo kimemfanya awe rais! Kweli Tanzania tumepata hasara. Ni aibu tupu kusema maneno ya kijinga kama haya yametoka kwenye kinywa cha rais wa nchi.
Huenda nchi yetu haina maendeleo maana kuna hii katiba iliyopo sasa, hivyo inatakiwa tusiwe na katiba kabisa hadi tuwe na maendeleo.
 
HUYO ATUELEZE KATIBA NININI??
Unapotaka kuongoza watu unavyojiskia wewe huwezi kutaka katiba Bora!!
Utateuaje MKWE wako kuwa waziri kama katiba haikupi nafasi yakufanya utakayo?? Watu wajinga wengi watakuabuduje? Utajilimbikiziaje Mali wewe na nduguzo??
Ili tupate katiba mpya inabidi kama taifa tuwe nawatu strong na conscious ( imara na wanaojitambua) kitu ambacho nishughuli maana wengi ni dhaifu na wasojitambua, wanajua kumsifu tuu kiongozi ili wapate chakula leo
 
Baada ya kuyasikia yote, niliishia kujisemea Nchi sio familia.
 
Ni kweli pale naona kama alipanic na akikosa hekima sema wanawake ni waropokaji.
 
[emoji2956][emoji120][emoji7][emoji1666][emoji106][emoji1720][emoji2788][emoji1732][emoji123][emoji95][emoji117][emoji109]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi....

Sasa ujenzi wa SGR umeletwa na katiba ?!!!!

Ile adha ya pale lilipo daraja la juu la "mfugale" iliondolewa na katiba ?!!! [emoji3][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Huko kichwani mwako kuna kila aina ya wadudu, maana kila kukicha kuna aina mpya ya mdudu anayejitokeza mbele na kushikilia wadudu wengine wote siku hiyo wasifurukute.

Huyu mdudu wa leo ndiye kakufanya uuone ujumbe huo kuwa wa maana zaidi wakati hauna chochote cha kuufanya uwe wa maana.

"Viongozi wa kisiasa tunadhani tuna haki ya kuburuza watu tunawageuza watu makasuku." Kuna lipi la maana katika mstari huu la kukufanya uone ujumbe ni bora sana katika mwezi wa September?

"Nenda kamuulize kifungu gani cha katiba kinakuudhi. Hajui" - Hili ndilo linalokufanya uone uzito wa ujumbe huo kuwa mkubwa sana kwako? Huyu mdudu wa leo huko kichwani mwako hutumia kilevi?

"Sasa katiba mpya ilete nini" Anakujibu "Maendeleo" Kuna lipi la maana hapa katika maneno haya kama siyo kuonyesha upungufu wa uelewa wa mtu aliyeyatamka maneno haya yanayokufanya wewe uone ujumbe ni bora sana wa mwezi wa September?

Baraza la mawaziri alilo nalo Samia limejaa wanasheria wasiojua maana ya sheria na katiba, au ni yeyye Samia kawafundisha kwa miaka mitatu waielewe Katiba na sheria ili wazitumie kama wanavyotaka kuwafundisha wananchi wote matumizi ya katiba hata hii mbovu wanayoikiuka kila mara wao?

Wanataka kwenda kuwafundisha wananchi namna ya kuitumia katiba kwa njia wanazotaka wao?
Hii ni katiba ya nchi, au ni katiba ya genge la wahuni waliko ndani ya CCM, wewe Johnthebabtist' ukiwa mmoja wao?
 
Katiba ndio mkataba mama isipokua vzr utazaa vimikata vibaya vingi vya kutuibia
 
Inasikitisha. Tuko pamoja
 
Mwanafalsafa mkubwa Plato alipendekeza hii kitu "philosopher king";na akaweka msisitizo thabiti kwamba lazima Kiongozi (king) awe ni mtu mwenye upeo mkubwa wa kiakili ambaye ataweza kubaini ukweli jinsi ulivyo (objective truth) na ukweli kama unavyojitokeza (relative Truth).

Ni kwa bahati mbaya kwamba taifa letu vilaza ndo viongozi na hili,lisha wahi kutamkwa na nguli wa fasahi Tanzania na Afrika Mashariki bwana Shaaban Robert "Kuna Karne itafika kwa wajinga kuwa viongozi na werevu kuwa wafuasi nadhani Karne yenyewe ndo hii".
 

Tunajaribu kusafisha eneo kuku kanya, mara bata anaharisha.
 
haya maendeleo anayoyawazia Samia, ambayo anajua hayaletwi na kitabu, yeye anaamini yataletwa na kunadisha mali zetu na kuwategemea hao wanaokuja watuletee maendeleo?
Hicho ndicho kitabu chake anachokiamini yeye kuwaondoa waTanzania katika hali ya maisha duni?

Anaamini, ni yeye na Baraza lake la Mawaziri wanasheria, ndio wanaojua na kushikilia funguo za kuwaletea waTanzania maendeleo bila ya kuwashirikisha wananchi?

Hotuba hafifu kabisa isiyokuwa na mwelekeo kwa nchi.

Haya ndiyo matokeo ya kuokoteza tu viongozi bila hata kuwa na njia zinazofahamika hawa watu wanaokotwa wapi.
Haya yote ni matokeo hayo hayo ya kuwa na katiba mbovu.
 
Katiba ni nini?
 
Ndiyo, maendeleo yanaletwa na kitabu. Kila jambo la maendeleo hupangwa kwenye kitabu ndio utekelezaji hufuata, mfano ni namba gani tutapata Rais, wabunge na madiwani imeandikwa, Ila CCM kwa uroho wao wa madaraka hukiuka na kupitisha wagombea kwa nguvu ya TISS na Polisi, kama ambayo watu tunavyokiuka vitabu vya dini na kuitwa Wadhambi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…