Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

amesema kweli tupu bila unafiki.
na huo ndio ukweli.
hata ningekuwa mimi ningefanya hivyohivyo.
 
Welewa wawatu ndoshida sasa mtu akiwa against nawewe utafanyaje naye kazi?
Kuwa na mawazo tofauti haimaanishi kuwa against namtu
 
Alisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimaja
 
Hili linazidi kuonyesha namna wapinzani walivyo wachochezi. Kilichoxungumzwa na namna kilivyo zungumzwa ni tofauti kabisa na mnavyokileta. Wekeni uchochezi pembeni tujenge nchi
 
Haya maoni yangetolewa na Magu akina Fatuma Karume wangeshachafua hali ya hewa hadi wale akina Anna Henga.
 
Ukisema ukali wa mtangulizi wake unaachaje kusema udhaifu wa JK ambaye aliligharimu mpaka taifa kutaka kuzama shimoni kwa rushwa, ubadhirifu, madawa ya kulevya, wapiga dili na hadi chama kutaka kumfia.

Aghalabu kwa ukali wa Magufuli tumeshuhudia nchi ikipiga hatua katika sekta nyingi ambazo huitaji tochi kuona, lakini tuliona uwajibikaji kwenye ofisi za serikali na uma.
 
Mama alipokuwa pembeni alimuona Magu kama mkandamizaji na asiyeheshimu taratibu.

Lahaula akachukua nafasi, akawarudisha watu wote ambao Magu aliwaweka pembeni. Wale waliotofautiana na Magu kwa namna yoyote akiwemo Mbowe akawaita ikulu. Akakutana na kila aliyepishana na Magu kutaka kuonyesha Magu ndio alikuwa na mapungufu.

Lakini kwa sababu muda ni mwalim mzuri leo tunashuhudia akitoa kauli tata. Ndio kwanza ana miezi 19 tu. Ameshaonja joto ya maumivu kutoka kwa watu wasiokubaliana na yeye na anajibu hadharani tena yupo tayari hadi kuvunja sheria za kimataifa ili kukabiliana na opponents wake.

Mwenzie Magu pamoja na mapungufu hayo ambayo hata Mbowe angekuwa rais angeyafanya kama ambavyo ukienda nae kinyume ndani ya chadema huchukui round utakiacha chama au kupotezewa mbali bado Magu aliperform.

Sasa yeye ni rushwa, ubadhirifu, pesa chafu, madawa ya kulevya, no umeme, no maji, huduma mbovu za kijamii. Lazima atajikuta ana maadui wengi.

Na huu ni mwanzo, ngoja tuone. Hivi bado anajibu meseji twitter.? Mwanzoni alipokuwa anajibu kuna rafiki yangu nilimuambia ni suala la muda. Nguvu ya soda.

Kuwa kiongozi wa nchi hasa rais kwa afrika ni kazi ngumu mno.
 
Mbowe alikamatwa kwa sababu hii. Hata sabaya anakutana na mkono wa mama kwa sababu hii hii. Ndugai je halafu wanatoka wanasema demokrasia imaimarika uongo mtupu
 

Nenda uka double deep maana, muktadha na mantiki ya neno upinzani. Pia tafiti zaidi kuhusu, watu wanaopinga lkn wanajenga kitu moja kama watafanikiwa.
Wazo la vyama vya upinzani lililetwa na mabeberu wa magharibi, na sisi kama ilivyo kawaida yetu ya kuiga kila kitu chao bila kufikiri, tukalimeza wazo hilo hivyo hivyo bila kutafakari kama linaweza kuendana na mazingira yetu. Matokeo yake ni matatizo juu ya matatizo. Imepita miongo mitatu tangu wazo la vyama vya upinzani liingie Tanzania na barani Afrika kwa ujumla, hakuna mafanikio ya kupigia mfano yaliyopatikana. Wazo la vyama vingi ni mradi uliokufa kwa Afrika. Siasa za Afrika zinaendana na misingi ya mila na desturi zilizojengeka katika nchi husika. Hivyo ni wakati muafaka kwa nchi na bara kwa ujumla kujitathimini kama mfumo huu una manufaa kwetu, au tuufanyie mapitio ili uendane na mahitaji yetu na wakati.
 
Haya maoni yangetolewa na Magu akina Fatuma Karume wangeshachafua hali ya hewa hadi wale akina Anna Henga.

Hii ndiyo aina ya upinzani tulionayo nchini na Afrika kwa ujumla.
 
Hivi hii ina uhusiano wowote na kufeli kwa wanafunzi katika LAW SCHOOL OF TANGANYIKA
 
Mbowe alikamatwa kwa sababu hii. Hata sabaya anakutana na mkono wa mama kwa sababu hii hii. Ndugai je halafu wanatoka wanasema demokrasia imaimarika uongo mtupu

Kweli kabisa naona Bashiru amesave.
 

Mbona huu mfumo unafanya kazi vizuri kwenye baadhi ya nchi zilozostarahabika.
Ghana, Zambia, Malawi, Kenya, South Africa, na Sasa Angola wameamka.

Nadhani shida sio upinzani ni mfumo wa vyama vingi kutokuwa na sheria inayoendana na mazingira yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…