Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimajaMh. Rais usianze kutupoteza hata sisi wapenzi wako ambao bado tunakutetea hata pale unapokosea wazi. Kumbuka umeanza vema kwa kuliunganisha taifa, sasa umesifiwa mgema tembo anaanza kulitia maji.
Kumbuka hata Hayati Magufuli alianza hivi hivi kidogo kidogo na mwisho wake wote tunaujua. Mama hii nchi ni yetu sote, hii nchi ni ya Watanzania wote.
Kwa leo naishia hapa mama, usiku mwema na Mungu akubariki.
Nimeufungua kwa haraka uzi huu, baada ya kuona kuwa nawe umechangia chochote!Bora,
P
Ukisema ukali wa mtangulizi wake unaachaje kusema udhaifu wa JK ambaye aliligharimu mpaka taifa kutaka kuzama shimoni kwa rushwa, ubadhirifu, madawa ya kulevya, wapiga dili na hadi chama kutaka kumfia.Mama kakosea sana, huo ukali ndo alikuwa nao mtangulizi wake matokeo yake mama mwenyewe ndo unamgharim kuweka mambo sawa na kuwafariji baadhi ya waliopitia magumu utawala wa mtangulizi wake.
Sasa hii nitawaba… kwa sheria za ndani sio nzuri wakati kimataifa unatafuta suluhu hiyo hiyo!
mf: ya kuchoma vifaranga kwa sheria za ndani.
Mi naamini washauri na watu wa karibu wa mama wanampoteza kwa sasa na mbaya zaidi madudu yanazidi kutokea na hakuna hatua zo zote anazichukua hasa kwa wasaidizi wake.
Mwishoni ataambiwa KAA PEMBENI HUNA MVUTO tuweke mwingine tukiokoe CHAMA kwanza!
Mbowe alikamatwa kwa sababu hii. Hata sabaya anakutana na mkono wa mama kwa sababu hii hii. Ndugai je halafu wanatoka wanasema demokrasia imaimarika uongo mtupuRais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake
Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.
Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.
Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.
Zaidi ya kupinga kwa maneno tu, huwa wanafanya nini kingine? Kwanini maneno tu mnayachukulia ubaya kiasi hicho kuliko ninyi wenye dola mnaofanya "vitendo" kabisa ambavyo vingi ni vya hovyo.
Kwanini mnaogopa kupingwa, mtu akikupinga anakusababishia nini?
Haya maoni yangetolewa na Magu akina Fatuma Karume wangeshachafua hali ya hewa hadi wale akina Anna Henga.
Hata Magufuli ana afadhali.
Huyu maza ni dikteta haswa aliyejificha kwenye ushungi
Hii ndiyo aina ya upinzani tulionayo nchini na Afrika kwa ujumla.
amesema kweli tupu bila unafiki.
na huo ndio ukweli.
hata ningekuwa mimi ningefanya hivyohivyo.
Kura za Bongo unaziamini?80% ya watanzania walikataa vyama vingi, endapo japo45 % wakikubali, maana yake hata bungeni ingekuwa 50 kwa 50
Mbowe alikamatwa kwa sababu hii. Hata sabaya anakutana na mkono wa mama kwa sababu hii hii. Ndugai je halafu wanatoka wanasema demokrasia imaimarika uongo mtupu
Maza naona madaraka sasa yameanza kupanda kichwani.
Nenda uka double deep maana, muktadha na mantiki ya neno upinzani. Pia tafiti zaidi kuhusu, watu wanaopinga lkn wanajenga kitu moja kama watafanikiwa.
Wazo la vyama vya upinzani lililetwa na mabeberu wa magharibi, na sisi kama ilivyo kawaida yetu ya kuiga kila kitu chao bila kufikiri, tukalimeza wazo hilo hivyo hivyo bila kutafakari kama linaweza kuendana na mazingira yetu. Matokeo yake ni matatizo juu ya matatizo. Imepita miongo mitatu tangu wazo la vyama vya upinzani liingie Tanzania na barani Afrika kwa ujumla, hakuna mafanikio ya kupigia mfano yaliyopatikana. Wazo la vyama vingi ni mradi uliokufa kwa Afrika. Siasa za Afrika zinaendana na misingi ya mila na desturi zilizojengeka katika nchi husika. Hivyo ni wakati muafaka kwa nchi na bara kwa ujumla kujitathimini kama mfumo huu una manufaa kwetu, au tuufanyie mapitio ili uendane na mahitaji yetu na wakati.