Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Arusha amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Samia anataka kujenga nchi huku anaogopa wapinzani, ndio maana mpaka leo bado hajaruhusu mikutano ya siasa, kumbe sababu anawaona wapinzani ni maadui zake.

Hii ni mentality ya kidikteta kabisa, utawatenga vipi wanaokupinga ikiwa nao ni watanzania, na uwepo na maoni yao vipo kisheria? anataka wanaomsifia tu ndio awaamini hata kama ni wajinga, kumbe ndio maana tunaogelea kwenye mgao wa umeme usiojulikana utakwisha lini.

Sasa wale kina Mbowe na Heche wanaohangaika kwenda kwenye vile vikao vyao ikulu naamini watakuwa wamepata jibu, ndio maana licha ya mazungumzo ya maridhiano karibia zaidi ya miezi sita, lakini bado work done is equal to zero.
 
Kasema ukikaa ki uadui..sio kila anaepinga adui...sio kila upinzani ni uadui ....adui ni Yule anaepinga kila kitu...mtu analalamika mgao ...akiambiwa tumenunua mitambo ya gesi kuondoa mgao hataki pia ..anataka tusubiri bwawa la Nyerere...sasa watu Aina hiyo ni wazalendo au wanafiki
Elimu tosha kwa wanaobwabwaja
 
Huyu mtu hata haelewi kuongoza serikali ni kitu gani.

Anafikiri ni vita.

Hawa watu wanapeea uongozi bila ya kuandaliwa vizuri.

Hawajui political economy theory, hawajui philosophy, hawajui politics.

Wanakuja kutawala by personal animosity.

Ndiyo maana hatuelewi maendeleo ni nini.

Yani achana na lengo la kuendelea, hata lengo la kuelewa kuendelea ni nini hatujalielewa.

Sasa tunategemea hili fupa lililomshinda Simba hawa fisi na mbwa wataliweza?
Tutafsiliye maneno ya lugha ngeni uliyoandika maana wengine hatujui hizo lugha ni kiswahili tu na kikwetu.
 
She is still far better than Magufuli..
At least utamtukana utaenda kulala bila wasiwasi....

Hakuna Ben Saanane kupotea
Wala Roma kutekwa wala Maxence Melo kushinda mahakamani...
Unakariri matatizo kama vile awamu hii hakuna tatizo, hapa nilipo hakuna umeme halafu unasema tushangilie tu na hili joto eti kwa sababu siku hizi hatutekwi!.

Hii thinking yako sijui ya sampuli gani, unadumaza upeo wa vijana wa hili taifa.
 
She is still far better than Magufuli..
At least utamtukana utaenda kulala bila wasiwasi....

Hakuna Ben Saanane kupotea
Wala Roma kutekwa wala Maxence Melo kushinda mahakamani...

That is a false dichotomy.

If she is stupid, she is stupid. It does nit matter how better than Magufuli she is. I did not compare her with Magufuli.

Pia si kweli kwamba utamtukana ataenda kulala bila wasiwasi.

Ana wasiwasi sana akitukanwa.

Haelewi kwamba kutukanwa ni sehemu ya urais. Ukubwa gunia la chawa.

Kama hutaki kutukanwa, usigombee uongozi.

Na unavyozidi kupanda juu matusi ndivyo yanavyozidi.

Kwa sababu unavyozidi kupanda juu ndivyo unavyozidi kuhudumia watu wengi, na ukihudumia watu wengi, haiyumkiniki kuwa utakosa wa kukutukana.

Maneno ya bandiko la awali hapa yanaonesha Samia is very petty and has some sort if inferiority complex inayompa wasiwasi wa kijinga akitukanwa na watu walio so far under her they might as well be shadows.

Sasa hivi badala ya kujikita kwenye ma deal makubwa ya kinataifa ya climate change tupige mabilioni ya dila za Kimarekani, anaenda kujiinesha anavyoogooa internal criticism.

She is acting like a silly little girl.
 
Back
Top Bottom