Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Arusha amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

That's Plain Truth!
 
Kasema ukikaa ki uadui..sio kila anaepinga adui...sio kila upinzani ni uadui ....adui ni Yule anaepinga kila kitu...mtu analalamika mgao ...akiambiwa tumenunua mitambo ya gesi kuondoa mgao hataki pia ..anataka tusubiri bwawa la Nyerere...sasa watu Aina hiyo ni wazalendo au wanafiki
Umeandika mataputapu sana....sasa kazi ya vyama vya upinzani ni ipi na ipi?
 
Sisi ndio uelewa wetu mdogo Rais anaongelea vyama vya kitaalamu hajaongelea vyama vya siasa kama unataka siasa unaingia katika siasa sio kujificha kwenye vyama vya kitaaluma nakufanya harakati. Adui yangu nimshirikishe kwa lipi? aje aharibu apinge kama mpinzani sio kujifanya chama cha wanasheria kama kina Lissu walivyoingia mle kuleta siasa.
 
She is still far better than Magufuli..
At least utamtukana utaenda kulala bila wasiwasi....

Hakuna Ben Saanane kupotea
Wala Roma kutekwa wala Maxence Melo kushinda mahakamani...
Huyu mama hana ubora wowote kumzidi Magufuli.
Kwanza hajiamini na ndiyo maana kila mwenye mtazamo tofauti na utendaji wake anamuona adui.
Hii nchi haiwezi ikaenda popote kama wote tutakuwa na mawazo yanayofanana.
Awe mvumilivu,asilikilize hoja za wanaompinga na azifanyie kazi.
 
Samia anataka kujenga nchi huku anaogopa wapinzani, ndio maana mpaka leo bado hajaruhusu mikutano ya siasa, kumbe sababu anawaona wapinzani ni maadui zake.

Hii ni mentality ya kidikteta kabisa, utawatenga vipi wanaokupinga ikiwa nao ni watanzania, na uwepo na maoni yao vipo kisheria? anataka wanaomsifia tu ndio awaamini hata kama ni wajinga, kumbe ndio maana tunaogelea kwenye mgao wa umeme usiojulikana utakwisha lini.

Sasa wale kina Mbowe na Heche wanaohangaika kwenda kwenye vile vikao vyao ikulu naamini watakuwa wamepata jibu, ndio maana licha ya mazungumzo ya maridhiano karibia zaidi ya miezi sita, lakini bado work done is equal to zero.
Kila akifungua mdomo namna hii anajianika ujinga wake.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Arusha amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Nimeipenda sana hii kauli. Ni muhimu tuwe wazalendo
 
Back
Top Bottom