Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Samia alikuwa na nafasi ya kuwa zaidi ya rais.Mama anataka wanaomsapoti kwenye Mbio zake za Urais 2025 tu.
Nje ya hapo hakuna.
Ni lini Ccm au viongozi wake walishamshilikirisha mtu mwingine kwenye mambo yake?
Rais Samia awe mwazi asizunguke zunguke mbuyu.
Inaonekana Mbio za Urais zinamtesa sana.
Alikuwa na nafasi ya kuwa kiongozi wa Africa na dunia.
Angeweza kuwa stateswoman.
Sasa hivi Africa haina rais mwingine mwanamke.
Ana nafasi kubwa ya kusikilizwa si kama rais wa Tanzania tu, bali mwakilishi wa watu wote, hususan wanawake kutoka nchi zote zinazoendelea.
Lakini kwa maneno haya ya shombo la taarab za mipasho, asahau kupata credibility.
Watu wanamsoma kimataifa na kuandikiana vimemo kwamba hapa hamna kitu.