Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Mheshimiwa Raisi sio lazima upate support ya kila mtu, heshimu na wasikilize wasiokubaliana na wewe wengi wao wanakuambia ukweli (ingawaje mchungu), chawa waliokuzunguka mara nyingi hawasemi ukweli, kalitazame hilo
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu...
Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.
Kwa msimamo huu yumekwisha. Baadae ya Tanzania imo gizani.
 
Muulize mange kimambi,, mwenyewe alinyooshq mkono,, ukweli ndio huo,, asilimia kubwa ya wananchi hawako tayari kubadili statu quo
Wangeweka uwanja sawa wa kufanya siasa na kuacha kutumia mabavu ya vyombo vya dola kuiba kura ndiyo tungepata jawabu sahihi.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake...
Imebadilika majuzi, nadhani learned friends walichoka kutumiwa. Wanaharakati wa CHADEMA walikuwa wakifaidi advisory fees makampuni ya makanikia huku wakijitia watetezi.

Msisahau CHADEMA hawajakata tamaa lakini, si walimfadhili Mtobesya awe Rais wa TLS afuate nyayo za tundulissu na fatmakarume?

Kura zikakata kutosha. Halafu partners wenziye fatma IMMA wakamfukuzilia mbali walipoona anawatia doa kampuni? Tulikuwa tuajiuliza hawa ni taaluma ya matusi?
 
Huyu huyu alipoingia madarakani akawadanganya chadema kwamba atateua wapinzani kwenye serikali yake, wakafikiri mbowe atateuliwa wakasema anaupiga mwingi.
Uongo, ameingia madarakani akiwa na agenda ya kumfunga Mbowe na kumalizia kazi aliyoiacha yule dhalim ya kusambaratisha upinzani.

Hiyo ya kuwadanganya Chadema kuwapa nafasi ni utunzi wako wewe. Ni matamanio ya kila mwanaccm kuona hakuna upinzani ili wanapofanya ufisadi wao asiwepo wa kuwakemea,Samia ni mwanaccm.
 
Kasema ukikaa ki uadui..sio kila anaepinga adui...sio kila upinzani ni uadui ....adui ni Yule anaepinga kila kitu...mtu analalamika mgao ...akiambiwa tumenunua mitambo ya gesi kuondoa mgao hataki pia ..anataka tusubiri bwawa la Nyerere...sasa watu Aina hiyo ni wazalendo au wanafiki
Mkuu huwezi kulazimisha upendo. Fanya majukumu yako ipasavyo na kutimiza wajibu maendeleo siyo Siri kila mtu ataona. Lakini kila kitu kinapopanda bei, ufujaji wa Mali unaoonyeshwa kwenye ripoti ya CAG haufanyiwi kazi unajua kuna mtu hatimizi majukumu yake.
 
Kwa hiyo chama cha wanasheria kwa miaka 4 nyuma walikuwa wanakosea?
Yes Mimi pia nilikua siafiki TLS kuhodhiwa na wanasiasa both wa CCM au Chadema. Najua ilikua strategy ya upinzani kuwa na sauti kwenye lobby groups ila wangeweka moderates sio extremists au active politicians kma Lissu/Masha/Karume n.k
 
Yes Mimi pia nilikua siafiki TLS kuhodhiwa na wanasiasa both wa CCM au Chadema. Najua ilikua strategy ya upinzani kuwa na sauti kwenye lobby groups ila wangeweka moderates sio extremists au active politicians kma Lissu/Masha/Karume n.k
Mbona sijawahi kuona ukipinga hilo?

Na ulikuwa unawashambulia kweli kweli waliokuwa wanataka tls isihodhiwe na wanasiasa?
 
Kwahiyo nchi kukosa umeme na maji ni kwasababu ya mfumo wa Nyerere?
Watoto wanamaliza shule hawajui kuandika wala kuhesabu vizuri,ni kwa sababu ya mfumo wa Nyerere...
Mimi siyo kiongozi wa nchi ila nauona mbovu alioujenga Nyerere unaotukwamisha. Miaka 60 ya uhuru maji na umeme bado changamoto, huoni kuna sehemu tumekosea hapo?
 
Back
Top Bottom