Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Raisi yupo sawa kabisa mafuta yamepanda na yanaendelea kupanda.Isiwe maisha yenu yapo kwenye wasapu tu angalieni huko ulimwenguni kuna nini ili msiipe shida sirikali.
Ila nimesikia Mafuta ya urusi yanapatikana kwa bei chee na wanakufikishia mpaka mlangoni achaneni na opec,ila ameshusha kwa nchi rafiki tu na kama haittoshi kuanzia kesho 31/03/2022 ,urusi haitapokea dola au pound katika biashara ya kimataifa watapokea rubo kama sijakosea.
Unajua na nyie Kuna muda huwa mnajishangaa wenyewe

Iliwekwa tozo mkashangilia na kusema serikali inapaswa kukusanya Kodi zaidi.

Mwezi uliopita tozo ikaoondolewa, mkasema ni Jambo zuri serikali kupunguza mzigo wa Bei kwa wananchi

Tozo imerudishwa mnasema Ni sawa kabisa

Mna tatizo gani lingine ukiachia hili la akili?
 
kusema kweli viwanda vya ndani asilimia kubwa" NI MZIGO"
wana maringo sana Bora vife tujue moja kuwa kila kitu tunaagiza kutoka nje.
True,vya ndani bei juu kuliko nje,check sement ilikuwa inatoka pakistan tena Ina ubora wa hali ya juu iliuzwa bei chee,sukari toka nje bei chee.

Unalinda nini Acha competition ifanye Kazi dhaifu afe,ndio mfumo wa duniani.
 
Hawana ubunifu wa kupata mapato wanachojua ni kutegemea kodi tu kwa kuwaumiza wananchi tu
Huo ndio ubunifu wenyewe.

Rais akitengeneza filamu mnaponda,akivutia wawekezaji mnaponda,akiweka tozo mnaponda akiwaambia mdai risiti mnalaumu.

You guys are mother fucker,na angekuwepo Mwendazake wote mungekuwa maskini afu muone moto.
 
In fact mimi niliwahi kupinga toka mwanzo Rais alipoanzaga kuondoa au kufuta tozo ya miamala ya simu kwa sababu tayari ilishakuwepo kwenye bajeti na isitoshe hicho chanzo kulikuwa specific kwenye afya, barabara,maji na elimu.

Unapoondoa manake unaharibu mipango ya serikali.

Kuhusu tozo ya mafuta,kwanza nilishangaa how comes uondoe tozo ya sh.100 ulivyosema ni ya Mfuko wa Tarura? Unaondoa wakati tayari umekomit miradi na wakandarasi wako site,utawalioaje kama sio kuwasababishia umaskini kwa sababu ya Madeni?

Hapo kwenye mafuta kuna Kodi za kuondoka kama tasac,TBS ,ewura na takataka zingine ila sio kuondoa pesa ya maendeleo.
Ww jamaa si ulikua unatoa sifa humu za kuondolewa hiyo tozo?

Tena ukamsifu waziri wa nishati na raisi

Hebu kuwa serious aisee
 
Wanaumeeeeeee
Screenshot_20220330-081209.jpg
Screenshot_20220330-081307.jpg
Screenshot_20220330-081251.jpg
 
Mama mpaka 2045,Tunampenda tunamkubali,impacts za kidunia zinagonga KILA taifa,

Labda katika utawala wake mama yetu aanzishe mpango maalumu wa ghala kubwa zaidi lenye kuweza kuhifadhi mafuta kwa miaka walahu miwili tu,thats how we can made country stability.
Napenda kuona hili linachukuliwa na serekali ili kujenga uimara Fulani Mara yanapotokea majanga ya aina hii
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe.

Rais Samia ametaka wananchi kuambiwa ukweli kwamba nauli zitapanda na usafirishaji wa bidhaa umepanda, gharama ambazo zitaingizwa kwenye bei za vitu.

Kuhusu bei ya mafuta ya kula ameomba tathmini ya tozo iliyowekwa kwenye mafuta yanayotoka nje ili kulinda viwanda vya ndani itazamwe tena kwani viwanda hivyo vya ndani havizalishi.

========

Rais Samia: Bei zimepanda kwa bidhaa nyingi tunazoagiza kutoka nje lakini kuna upandaji wa bei za mafuta, mafuta yamekuwa yakipanda nadhani kutoka mwaka jana katikati ya mwaka.

Tukachukua hatua ya kupunguza tozo ndani ya mafuta kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi lakini mafuta yameendelea kupanda.

Kipindi hiki cha pili mafuta yamepanda kwa 156 kwa lita, waziri akaona nikitoa shilingi mia yapande kwa shilingi 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge kwahiyo kulikuwa na utata kidogo, tumekaa kama Serikali tumerekebisha.

Ile shilingi iliyotoka, nimeagiza irudishwe na tathmini tuliyofanya hata kama ile shilingi tungeitoa, kwa mwenendo wa upandaji wa mafuta duniani, bado isingekuwa na impact ila tungejikosesha kile ambacho tunakifanya, kwahiyo tumeamua shilingi irudishwe.

Wabunge wenye maeneo yenu, mawaziri mnaosimamia sekta waambieni wananchi ukweli, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na mafuta yanapopanda ndio kila kitu kinapanda.

Nauli zitapanda, usafirishaji wa bidhaa zitapanda. Sasa hivi kutoa kontena China ya bidhaa kuleta Tanzania walikuwa wanalipa kontena ya ft 40 dola 1500, sasa hivi ni dola 8,000-9,000. Hii inaenda kuingia kwenye bidhaa anazozileta kwahiyo waambieni wananchi ukweli, wasikae tu kulaumu Serikali haisemi kitu.

MAFUTA YA KULA
Rais Samia:
Nakumbuka nilikuagiza waziri wa fedha kwamba katika bajeti yetu tunayoimaliza tuliingiza kitu katika mafuta ya kula nadhani na ya nyuma yake ili kulinda viwanda vya ndani nadhani kwenye uzalishaji lakini pamoja na kuongeza hiyo kitu kuzuia mafuta ya nje yasije, viwanda vya ndani ndio vimefungwa kabisa hata huo uzalishaji wenyewe, kwahiyo naomba litizameni tena.

Kama haitusaidii ondoeni ili mafuta ya nje yaingie angalau hata kama bei itakuwa kubwa lakini wananchi wana mafuta ya kutumia. Sasa mmezuia ya nje hayaingii, ndani hayazalishwi, wananchi wanapiga kelele bila shaka mafuta yatapanda bei kwa kiasi kikubwa, nendeni katazameni vipengele vitakavyoleta unafuu kwa wananchi.

=> Kwa mfano kwenye bei ya mafuta Afrika Mashariki na kati Tanzania ndio ina bei ya chini kabisa ya mafuta lakini wenye sekta hawasemi, wamekaa tu wanajifungia.
Bibi eee wewe rudisha shillingi kwenye mafuta ila ondoa ile tozo mliyoweka kwenye miamala ya simu.

Pesa za tozo hatujui zinafanya kazi gani sasa maana misaada na mikopo tunapewa kila siku mara kutoka un, eu, usa, waarabu ......
 
Back
Top Bottom