Rais Samia: Sasa Tanzania tumeuza (Bandari), wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

"Wakati sisi tunalumbana bandari apewe nani iende isiende, ikae, ivue isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wame-jump wamekwenda kulekule, lile lile jumba lilowekwa bendera ya Tanzania limewekwa bendera ya jirani, sasa Tanzania tumeuza wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?, na siku ambayo bunge letu lilisema ni ruhusa bandari iendeshwe na serikali na sekta binafsi siku ya pili wenzetu wakasema nyinyi moja, sisi zote ziende private sector wakakimbia kule kuwahi nafasi,"- Rais @samia_suluhu_hassan

"Sasa muone jinsi ambavyo fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka, nilisema nitoe tu mfano huo kuona changamoto na jinsi ya kuzitumia fursa na kuzifanya zisichomoke,"- Rais Samia


#ViapoIkulu
#EastAfricaTV
 

Attachments

  • FB_IMG_1689343864760.jpg
    55.1 KB · Views: 3
Kwa nini Picha ya Bango la Rais wa Tanzania Dubai kwenye mnara mrefu pale Dubai lilikuwa na picha ya Rais wa tanzania bendera ya nchi yetu?

Ikumbukwe vyote hivi ni Mali yetu watanzania ndio maana uwezi chukua bendera ya Tanzania ukaibandika chooni ukawa salama.

Kwa nini Kenya imebandikwa ya nchi Yao na sio rangi ya Rais wa Kenya?

Tutachambua kila kitu no stone will be left unturned.
 
Mm na familia hatuja kataa wawekezaji tatizo ni aina ya mkataba. Yani mkataba hausemi wanapewa kwa mda gani yani miaka mingapi?
Watanganyika tucdanganyike na Maneno hayo.
 
Mama hajatuelewa kwa nini?

Sisi nani kamwambia tunakataa wawekezaji?

Kwa nini anaona ugumu kuelewa kinachopingwa ni aina ya mkataba na sio mwekezaji?

Nchi ngumu sana hii!

Korona pumbafu zake kabisa!
Aina ya mkataba ndio wa kisasa, mbona JPM alisaini mkataba wa bomba la mafuta, uliwahi kuuona unafananaje?.

Huu sio wa kwanza kusainiwa na wanasheria wa serikali, suala la bandari linagusa maslahi ya wafanya biashara wanaozoea kula pesa ndefu hivyo wanaona ni vigumu kuachia ulaji uwaponyoke.
 
Vifungu vipi vinasema hayo?
 
hiki kibibi bogus kabisa hiki, kwani wale wamesaini mkataba wa kipumbavu kama huu wetu?

nani anamshauri huyu bibi? huyu alistahili kuwa mchambawima kulea wajukuu
 
hiki kibibi bogus kabisa hiki, kwani wale wamesaini mkataba wa kipumbavu kama huu wetu?

nani anamshauri huyu bibi? huyu alistahili kuwa mchambawima kulea wajukuu
Mkataba upi wa kipumbavu? Una upumbavu gani?
 
Rais Samia tunamwomba atuelewe vizuri. Hatuna nongwa naye. Tena sisi wengine ni kati ya watu tuliokuwa mstari wa mbele kumpongeza katika mengi. Na sisi wengine tumefanya kazi mataifa mbalimbali kama sehemu ya management ya makampuni makubwa ya uwekezaji.

Haiwezekani kabisa tukapinga uwekezaji. Tunahitaji sana uwekezaji na wawekezaji lakini uwekezaji wenye tija. Huko tulikokuwa tukifanya kazi, tumeona wananchi wa mataifa hayo wanavyonufaika na rasilimali zao kutokana na uwekezaji wenye tija kupitia mikataba mizuri na mazingira mazuri ya uwekezaji.

TATIZO NI CONTENTS ZA MKATABA. TATIZO SIYO UWEKEZAJI. HATUGOMEI UWEKEZAJI HATA KIDOGO. KAMA HUKO SERIKALINI HAKUNA WATU WENYE UPEO WA KUTENGENEZA MIKATABA YENYE TIJA, OMBENI USHAURI HUKU NJE. KUNA WATU WENGI SANA.
 
waende na kawafuate kama unataka, wale ni wasomi na wanauzalendo na nchi yao hawawezi ingia mkata mbovu kama huu wa kwetu
 
Who's is fu.ckin.g johar in this country!?Wasomi wote waupinge then tuwapuuziie , halafu ndio tumsikilize mjinga mjoja sujui anaitwa johari!?
Kwa akili hizi hata mkielimishwa kuhusu vipengele vya mkataba ni kupoteza muda tu. Nilimuelewa sana JPM hakulea vichwa vya aina hii, mikataba mingi aliingia akiwa rais na hakuna hata mmoja tuliojadili kama huu wa bandari.
 
Siyo kwamba hawajui kinachobishaniwa. Wanajitoa ufahamu makusudi tu. Walete hapa IGA ya Kenya kama nayo itakuwa na Mkataba wa milele Kwa wa kwetu. Watu gani rigid hivi hamtaki kukubali mmekosea mkasahihisha?
Hakuna aliyekosea, hao walioshiriki kuiandaa hiyo IGA ni waalimu wa sheria kina Dr Possi na Hamza, usidhani ni wajinga wajinga tu waliokotwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…