Rais Samia: Sasa Tanzania tumeuza (Bandari), wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

Mkataba una shida gani?
Ni kama akili zenu nyote, wewe pamoja naorodha hiyo iliyokupa 'like'; akili zenu zimeganda mahali fulani na kamwe hamuwezi kuziondoa kwenye mgando huo.
Kama hadi wakati huu bado unauliza swali hilo, ina maana huamini kuwa hiyo 'IGA' ni mkataba.
Lakini pamoja na tunapokubaliana juu ya hilo, kuwa ni "Makubaliano", bado hamuoni ubovu uliomo kwenye hayo makubaliano!

Kinachotakiwa sasa, labda elekezeni akili zenu kwenye kuwaeleza wananchi wa nchi hii, kwamba "Makubaliano" hayo hayana uhusiano wowote na "Mikataba" itakayoingiwa.
Hapo mtakuwa na kazi ya kuwaambia wananchi kuwa makubaliano ya IGA yawepo au yasiwepo, haiathiri chochote katika mikataba hiyo ya HGA.

Kwa hiyo, nwasihi sasa, muelekeze akili zenu katika kuifuta IGA, ila tuendelee na HGA.

Nimeona mahali fulani ume'ni'quote', sijakusoma huko, nitakutafutia muda, maanake najua utakuwa umeacha takataka kama hizi unazoeneza kila mahali. Kwa hiyo vuta subira juu ya hilo.
 
Huyu mama uyu, why unasaini mkataba kimia kimia, ajipange hii ngoma nzito sana
Hakuna lolote, mikataba husika itasainiwa, DP WORLD atakuja , badabri itaboreka , na wapingaji wataaibika
 
Yaani huyo mama tunamheshimu sana ila ana shindwa kuwa na uelewa na vitu vidogo sana. Hakuna mtu ambaye hataki privatization ya bandari zetu kuongeza mapato na ufanisi. Ambacho hatutaki ni hio mikataba ambayo yeye anapewa huko akiwa kashashiba iftar. Afanye review ya mikataba iwe standard alafu aone kama kutakuwa na kelele. Vitu very simple vinamshinda.
 
Watakuja watakaa hapa wataiacha Tanzania ikiwa hoi ,tuona kama kutakuwa na change zozote kuwa mwarabu anatupenda sana
 
Akwende zake huko. Hatu copy na ku paste. Tunaishi Kwa katiba na Sheria.
 
Sitaki kuamini kwamba mama mpaka Sasa anashindwa kuwaelewa watanzania wanapinga nini au kwasababu hana la kujibu ndiomana kaongea hiko alichoongea kweli?🙆
WATANZANIA HAWAPINGI UWEKEZAJI BALI WANAPINGA AINA YA MKATABA TULIOINGIA NA HUYO MWEKEZAJI MWENYEWE.
Mama your office is too higher na inapaswa ikate kiu ya watanzania, nini hasa kinachoshindikana kuifanyia Reformation huo mkataba na kuondoa hivyo vifungu vinavyopigiwa kelele?
Kingine kweli mama swala la jumba refu duniani kuweka bendera ya Egypt ndio iwe bakora kwa kuwasuta watanzania? Kwani watanzania wanahitaji kupeperushiwa bendera yao kwenye hilo jumba au mazingira salama na mazuri juu ya rasilimali zao? That was too cheap for you to say in front of Camera😭
 
Je, kuna ukweli kuwa Nchi za Uarabuni, zinatumia uwezo wa DPW kuendesha bandari kumiliki rasilimali za nchi ugenini? Msikilize mchambuzi huyo


Ni kweli ndiyo maana makampuni makubwa huamua kununua kampuni ndogo zinazochipukia ili waondokane na ushidani au kunyakua fursa ambazo kampuni kubwa hawakuziona mwanzo .


Famed investor Warren Buffett has long talked about the importance of firms creating an “economic moat” around themselves as a way to stave off competition. But many of the tricks and strategies companies employ to get there are quite ugly and unfair and really tip the playing field. https://www.vox.com/the-goods/how-big-business-exploits-small-business
 
Hiyo bendera nasikia imeyeyuka
 
Unajua hakuna haja ya kukimbilia kusaini vitu vitavyoweka nchi kwenye matatizo.

Tuhahitaji wawekezaji, ila masharti yawe rafiki kwa maslahi ya Tanganyika na vizazi vyao huko mbele. Tusiuze nchi jumla sababu ya desperation.

Everything should be careful considered, without haste.
 
JPM alisaini mikataba ya bomba la mafuta mingi tu na ile mikataba ilisainiwa taifa zima tukishuhudia huku tukielezwa contents na kila hatua.

Mambo mengi ya kimsingi yahusuyo maslahi ya kitaifa aliyafanya live na kuyafafanua.
 
Mkuu ni kweli kabisa, wale Viongozi wetu wa kwanza baada ya kupata Uhuru walikuwa committed kwa Wananchi na maendeleo ya Nchi zao. Umenikumbusha ishu moja miaka ya 1970/80 Kampuni ya UDA ilipo kwenda Hungary kununua mabasi ya abiria aina ya Ikarus ambayo ni kama haya ya mwendokasi ; yule officer aliye enda kununua hayo magari aka zawadiwa "Ikarus moja fupi/dogo kama 10% yake, lakini Serikali lilimtaka Ofisa huyu arudishe bus hilo UDA, maana hiyo % ni kwa wa-TZ wote.
Viongozi turudi kwenye uzalendo huo.
 
UPOFU WA NGAWILA
 
Leo nimemsikia japo Kwa Mbali na Huwa sipendi kumsikia anaongea nini, Kwanza anatia huruma . Pumzi imekata kabisaa na wasaidizi wake wanazidi kumdanganya.

Nilitegemea nimsikie akitoa ufafanuzi Kwa Nini aliingia mikataba wa hovyo kama ule. Baadala Yake karudia ngojera zilezile eti tutapata faida.

Nilichosikitisha Zaidi ni yeyé kutoa mfano eti wenzetu wamekimbilia huko, whaaat kwa hiyó DPW ni Maembe ya bure tuyakimbilie kichwa kichwa bila kujiuliza.

Samia kafail pakubwa sana
 
JPM alisaini mikataba ya bomba la mafuta mingi tu na ile mikataba ilisainiwa taifa zima tukishuhudia huku tukielezwa contents na kila hatua.

Mambo mengi ya kimsingi yahusuyo maslahi ya kitaifa aliyafanya live na kuyafafanua.
Walioipitisha hiyo mikataba ni hawa hawa kina Hamza Johari ambao leo wanaonekana ni wasaliti kwenye nchi yao!, ndio uishangae Tanzania.

Chuki za kumnyanyapaa rais na waziri Mbarawa zinaonekana zina mantiki awamu hii kwa suala hili la DPW wakati wanasheria waliopitisha mikataba ya JPM ndio hawa hawa wanaofanya kazi na SSH.
 
Leo hakuna Mtawala wakuuuliza wala kukemea ubadhirifu wowote unaofanywa, maana hata neno RUSHWA hawataki kulisikia, wanataka wasikie neno TAKRIMA., ni ngum sana kuisha machafuko Nchi za Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…