Rais Samia: Sekta binafsi ndiyo itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara

Kama ni usimamizi, watawezaje kuwasimamia hao wawekezaji ili waweze kupata Kodi zao stahiki?
Hakuna haja ya kusimamia wskubaliane pesa kamili mwekezaji apate hasara au faida lazima alipe hapo ndio hutaibiwa mapato sasa ni 1.6 trillion tsh kwa hiyo aanza na trillion 2 kwa mwaka baada ya miaka mitano iwe trillion 7 kwa mwaka baada ya miaka mitano iwe 7 plus 10 percent interest kwa mingine mitano itakuwa 15 alafu tukae tuzungumze vipi biashara
 
Mkataba utakuwa ni mzuri zaidi ya unavyofikiria. Ni win win situation.
 
Aliyekwambia hatuangalii mkataba ni Nani? Serikali ya Samia sio ya kipuuzi mpaka ishindwe kufanya mikataba mizuri!
Sasa kama ni kweli kwanini watishe watu wakati wahusika wapo wasijitokeze wakaeleza kama kuna opotoshaji kuondoa taharuki maana hii nchi no ya watanzania na kama kuna taharuki sioni tatizo liko wapi kwa wahusika kujitokeza wakaweka ukweli wazi wazi.
 
Nilikuwa mtoto,ila ninakumbuka mama zangu kuwasikia wakisema Tanesco ilibinafisishwa kwa wasouth.Sasa sijui kilitokea nini ikarudi kwa serikali.Ila nadhani mikataba ilikuwa ina masharti ya kuvunjika kirahisi.
TANESCO haikubinafsishwa bali uendeshaji wake ulikabidhiwa kampuni binafsi kwa muda mfupi. Ilipoonekana ufanisi haujaongezeka mkataba ukasitishwa.
 
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Rais ni akili ndogo! Yaani unaita kampuni ya serikali nyingine, wewe unaitoa serikali yako ktk biashara! FOOOOL!
 
Anazungumza utadhani ni mhadhiri wa chuo anatoa lecture. Maneno yake ni mepesi mno na hayastahili authority ya cheo cha Urais.
 
Vibwengu vyake mabegani vimenyutiwa.
Lugha anayotumia, haina tofauti na lugha za kale za kibeberu. Mmeshamsahau Benjamin Mkapa? Tayari?

Tafsiri yake ni kuwa, tunahitaji Wazungu na Watu wa nje kuja kutufanyia Biashara?

Tanzania inayo sekta Binafsi, lakini ukitizama uwiano wa ulipaji wa kodi utakuta Sekta binafsi Tanzania(wazawa) ndio wanaolipa au ndio wenye mzigo mkubwa wa kulipa kodi! Huku Sekta Binafsi(wawekezaji au wazungu au FDI)za wageni, ndio wanaowezeshwa, yaani kila sikua utasikia "sheria au sera rafiki" kuongeza wawekezaji zikiwanufaisha wao tu....huku wakikingiwa vifua na Serikali zao! Huku kwetu mpaka Kariakoo wakaamka????

Nashindwa kuandika.....ila....

CCM must go!
 
Sasa kama ni kweli kwanini watishe watu wakati wahusika wapo wasijitokeze wakaeleza kama kuna opotoshaji kuondoa taharuki maana hii nchi no ya watanzania na kama kuna taharuki sioni tatizo liko wapi kwa wahusika kujitokeza wakaweka ukweli wazi wazi.
Nani katishwa au kukamatwa? Hayo ya kukamata ni mawazo ya musukuma na serikali mpaka dakika hii haijayafanyia kazi so nyie endeleeni kujadili tu na hizo taharuki zitaisha make chama na serikali inaendelea kutoa ufafanuzi so relax my dear friend!
 
Sakata la bandari ni kielelezo tosha public support kwake imepungua watu wanatafuta sababu tu ya kumlaumu ata pasipo na makosa.

Busara ni kuacha kusikiliza mipango ya tozo; ni bora kuacha kujenga hizo barabara kama hana uwezo kuliko kujiingiza kwenye miradi ya toll roads watu washachoka malipo.
 
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”

Alisema Rais Samia

Rais SSH ,na Rais hatutaki kuuza nchi kwa kisingizio cha sector binafsi kukuza uchumi ,watanganyika hatutaki , sector binafsi kwa mikataba kifisadi kama sio ya kipuuzi , sasa jidanganye kwamba upo na watu royal na hakuna wakufanya kitu , acha kabisa wewe ni rais ila nyoyo za watu mil 60 sio miliki yako

Umekua na ujasiri ambao umevuka mstari mwekundu, kama mmeshindwa tumia rasilimali za nchi kwa manufaa mapana ya taifa hili ziache zilivyo ,

unaweza ona upo na watu unawautubia ila ujui nyoyo zao zinakuona vipi thats haya mambo yamekua public tofauti na matarajio yenu,

Back
Top Bottom