Ndugu zangu Watanzania,
Tundu Lissu amesema ya kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge hajakosea kumuita Simba.
Amesema ya kuwa yeye amezaliwa kwenye ukoo wa Mashujaa wa Kinyanturu ,watu ambao wamewahi kuuwa Simba wala Ng'ombe na wezi wa ng'ombe wao. Amesema Mashujaa hao walifahamika kama "ahomi" au "Muhomi' kwa umoja.
Lissu Ameendelea kusema ya kuwa Babu yake mzaa baba yake amewahi kuuwa Simba aliyekuwa amevamia na kuuwa Simba. Laini pia hata Baba yake Mzazi naye amewahi pia kuuwa mara mbili Simba aliyekuwa amevamia na kuuwa Ng'ombe wao.
Chanzo cha habari yangu ni Gazeti la Kiswahili la Mwananchi la mtandaoni.kwa hiyo kama unataka kupata habari hii kwa undani nenda kanunue gazeti la Mwananchi kesho asubuhi na Mapema sana upate mambo mbalimbali ya moto moto.lakini pia waweza kulisoma mtandaoni kwa kulipia kiasi kwa kadri ya uwezo wako
Mwisho pia napenda kuwashaurini tena watu wenye uwezo wa kifedha jitahidini kuwapa hata vijisenti uongozi wa Jamii forum kama mchango utakao wasaidi katika mambo mbalimbali kama vile ulipaji wa billi za umeme ,maj n.k au hata kununua vifaa vingine watakavyoona vinafaa katika kuleta tija zaidi,maana mtandao huu una mchango mkubwa sana chanya hapa nchini.japo kuna wengine huwa wanautumia vibaya kwa kuporomosha matusi na kuleta habari za uongo na uzushi ,japo nashukuru sasa kuna jamii check katika kuhakiki habari.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.