Rais Samia: Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa

Rais Samia: Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa

Huwa naona viongozi wa dini wanaijua siasa zaidi kuliko wanaojiita wanasiasa.
Wafuatilie viongozi wa dini,utagundua mengi sana
 
Nilikuwa mbele kumshabiki huyu mama,lakini sasa naona anakokwenda siko na anaelekea kukwama totally
 
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 Mjini Morogoro wakati akifungua mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) aliposema wakati mwingine dini na siasa vinaenda sambamba....
Hapo kwenye kodi hapo, hapana! Mashirika ya dini yaendelee tu kulipa hiyo Income Tax, otherwise tutakwama...
 
Wapi imeandikwa? hajui kuwa siasa na dini hazitengani, vipi huko kwao Zanzibari dini na siasa unaweza isemeaje? inatambua makundi ya wachache? inatambua uhuru wa maamuzi kwa wachache? anafahamu kama msingi wa dini ni siasa pia?
 
Rais Samia amewataka viongozi wa dini kuacha kutumia dini kufanya siasa kwani jambo hilo siyo sawa.

Rais Samia amesema siyo vibaya kwa viongozi wa dini wa kuwa wanasiasa lakini ni jambo baya kwa viongozi wa dini kutumia dini zao kufanya siasa.

Source: ITV habari

Nawasalimu kwa jina la JMT.
Dogo si uwe unapumzikaga?
 
Akina bagonza hao , kila sku kurelate mafungu ya biblia kujipatia umaarufu kisiasa.....naona mama anaupiga mwingi sana
Umepungukiwa uelewa. Leo hii hukumsikia Samia akinukuu vifungu vya biblia? Kwa hiyo amwtumia dini kufanya siasa?
 
Mama anajilika sana na makafiri aisee
🤣🤣🤣🤣🤣

20210708_161632.jpg
 
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 Mjini Morogoro wakati akifungua mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) aliposema wakati mwingine dini na siasa vinaenda sambamba...
Hahahaa wale wapiga mayowe wamesikia.
 
Wapi imeandikwa? hajui kuwa siasa na dini hazitengani, vipi huko kwao Zanzibari dini na siasa unaweza letu isemeaje? inatambua makundi ya wachache? inatambua uhuru wa maamuzi kwa wachache? anafahamu kama msingi wa dini ni siasa pia?
Taifa letu bora limetenganisha DINI NA SIASA....na huo ndio ubora wenyewe......

Ziko nchi HAZIJATENGANISHA HAYO.....

#KaziIendelee
 
Hili halijakaa sawa... Dini na siasa visichanganywe...
 
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 Mjini Morogoro wakati akifungua mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) aliposema wakati mwingine dini na siasa vinaenda sambamba.

Amesema licha ya kuwa unaweza kutumikia dini na kuwa mwanasiasa, lakini vibaya unapotumia siasa kwenye dini. Amewaomba viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika kudumisha amani na usalama wa nchi uliopo.

Amesema ni nafasi ya viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yakitaifa ikiwemo suala la kuhesabiwa sensa linalotarajia kufanyika mwezi Agosti mwakani.

"Nawasihi viongozi wa dini kuwasihi wananchi kuachana na imani potofu na kushiriki kwenye sensa, suala la sensa lipo hadi kwenye vitabu vya dini na hivyo sio suala geni kwetu," amesema.

Rais Samia pia amewataka viongozi wa dini kote nchini kuhubiri amani, upendo na mshikamano huku wakizidi kuliombea Taifa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Katika risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT), Baba Askofu Dk. Alinikisa Cheyo, ameomba serikali kuondoa kodi ya mapato (Income Tax) kwenye shule na huduma za afya zinazotolewa na taasisi za kidini nchini.

“Tunaiomba Serikali ifikirie kuziondolea Taasisi za kanisa kodi za mapato (income tax) ili taasisi hizo ziweze kujiendesha kwani hazipati faida kubwa na ile faida ndogo inayoipata inatumika kughramia uendeshaji wa huduma hizo,” amesema Askofu Cheyo.

Chanzo: Nipashe
Sifa kuu za mwanasiasa ni udanganyifu, fitna, undumila kuwili, uchoyo wa madaraka, tamaa ya fedha na mali

Kazi kwenu viongozi wa dini
 
Back
Top Bottom