Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Awamu ya tano, Rais wa sita.
Awamu ya tano ktk utaratibu wa nchi yetu kuwapata viongozi haijaisha.
Kuna makitu hapa hayaelewi somo..kilichotokea ni sawa na useme mwanafuzni wa darasa la tatu...hakuendelea na masomo baada ya kuumwa mwaka 2020, anakuja kuendelea na masomo mwaka 2021 hii haimpi nafasi ya kurukia darasa la nne..wakati la tatu hajamaliza..so ataendela pale alipoishia
 
Kauli mbiu ya awamu ya sita ni ipi?

kila awamu ina kauli mbiu yake.

mfano Ujamaa na Kujitegemea Nyerere.

Ruksa mzee Mwinyi....

Uwazi na Ukweli Mkapa.

Hari Mpya Kasi mpya Kikwete.

Hapa kazi tu Magufuli
Suala la kauli mbiu haliko kwenye katiba, na hata anayeweka kauli mbiu anaweza kuibadili hata mara kumi ndani ya awamu yake.
Jk alianza maisha bora kwa kila Mtanzania,
Alipoona kachemka akaja na kasi mpya.....
 
Nimemsikia hata mimi,ila inatafakarisha kweli kweli.Maana awamu ni miaka mitano,na Rais wa kila awamu huwa anachaguliwa kwa sanduku la kura.

Mimi nilidhani huyu ni Rais wa sita, ila awamu ni ya tano!Labda tungepata ufafanuzi wa kisheria kutoka kwenye vyombo vyetu vya sheria,maana nilisikia mwanasheria mmoja aliyekuwa amealikwa TBC akisema hii ni awamu ya tano.

Anyway ni ya tano au ya sita sio issue sana,wananchi tunachotaka ni kupiga hatua kimaendeleo.
[IMG alt="areafiftyone"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/407/407721.jpg?1595674912[/IMG]

areafiftyone

JF-Expert Member​

Jan 4, 2017 8,669 2,000

Nimemsikia hata mimi,ila inatafakarisha kweli kweli.Maana awamu ni miaka mitano,na Rais wa kila awamu huwa anachaguliwa kwa sanduku la kura.

Mimi nilidhani huyu ni Rais wa sita, ila awamu ni ya tano!Labda tungepata ufafanuzi wa kisheria kutoka kwenye vyombo vyetu vya sheria,maana nilisikia mwanasheria mmoja aliyekuwa amealikwa TBC akisema hii ni awamu ya tano.

Anyway ni ya tano au ya sita sio issue sana,wananchi tunachotaka ni kupiga hatua kimaendeleo

Kweli umesema kweli na hata huyo Mwanasheria kasema vyema kuwa tupo Awamu ya Tano ila tumepata Rais wa sita kwa sababu hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ibara ya 37 (5) inafafanua kuwa Makamu anapoapishwa kushika nafasi ya Urais kumalizia kipindi kilichobaki cha Mtangulizi wake aliyefariki dunia au aliyejiuzuru au ni mgonjwa kiasi kuwa hawezi kumudu kazi yake ya urais basi haiwezi tena kuwa awamu nyingine ila inakuwa awamu ile ile tu.
 
Mzee..hivi unasoma katiba ama unafikiri kwa kutumia makwapa!? Haijalishi kuendelea ama kutokuendelea kwake..awamu huwa inahesabiwa kwa.miaka 10 ,mitano ya kwanzA na mitano ya pili ...ndio awamu inakuwa imeisha...kasome katiba uieleewe
Hahahaha mm sio mzee
Halafu Sina muda was kubishana
Utabaki peke yako unasema awamu ya tano wenzio tuko ya sita
 
Naona unachanganya matikiti na matango,tunaita awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kutokana na kuwa kwa kipindi chote cha utawala wake yeye ndie alikuwa raisi pekee na ndio maana tunasema kipindi cha utawala wake wote awamu ya kwanza,alipokuja Mwinyi katawala miaka 10 hiyo ni awamu ya pili na vivyo hivyo kwa kipindi hiki ni awamu ya tano hadi 2025 ndio atakayekuwa raisi atakuwa wa awamu ya sita. Mambo ya kusema tukiwa huru ni yako na familia yako Tanzania tumekuwa huru kuanzia 1961 pale bendera ya mkoloni iliposhushwa na bendera ya Tanganyika ikapandishwa juu tena kileleni mwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Nyirenda.
Hiyo awam umeitoa wapi?
Ni mawazo yako mfu na familia yako kuamini kua sijui kura na mambo mengine baseless ndiyo awamu. Awam ya tano imekua terminated kwa tukio natural baada ya mzee kuaga dunia, na uzuri wake mama Mungu akipenda atahudumu kwa miaka zaidi ya 3 ambayo kisheri inampa wigo mmoja tu zaidi yaani baada ya miaka hii minne na zaidi, anaruhusiwa mara moja tu kugombea ili kukamilisha ratiba ya awam yake ya sita na si vinginevyo. Wewe shupaza shingo ila mama ni Rais wa awam ya 6,hiyo ya 5 ni ya kwako.
 
Tumuongezee miaka kumi tubadili katiba
 
Hii niawamu ya tano inawezekana hata prez. hajui, hakujawa na uchaguzi wowote nimabadiliko tuu yauongozi Ila tunatembea na ilani ileile awamu ileile!

Huyu amekuja kivingine anageuza ya alompa kijiti tunaomba walosifia ya yule wakosoe yahuyu tabia ya ukinyonga muache kama ninyi kijani bakini na umajani wenu acheni unaa.

Ila tunamwambia kabisa kama wao zenji walipata katiba nasisi tunahitaji katiba nzuri,wao nchi sisi ninini? Katoka nchi yake amekuja kutuongoza tusojielewa nikamtaa ama nini? Nchi yao inamaprez wawili kivp sisi tutatetewa nanani? Uchaguzi huru vp?

Ngoja tuone ila neno tusahau hatulihitaji kwakweli!!! Yeye nawaziri wakatiba walikuwa wanachezea kodi zetu zams zile? Basi warudishe pesa zote walizogawana bunge la katiba.
 
JPM aliongoza serikali ya awamu ya tano, Je, Mama Samia anaongoza serikali ya awamu ya ngapi?
Je, ni nini kinachotenganisha kati ya awamu moja na nyingine?
 
Awamu inatenganishwa na kiongozi maana awamu ya kwanza mwalimu aliongoza kwa miaka 24, Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete kila mmoja 10, awamu ya 5 miaka 5 na hii ni awamu ya sita.
 
Ikulu ya Samia,kama wanavyosema Marekani,"Biden While House'.

Wakazi ,wapangaji,watu wa Ikulu wakibadilika,sera zitabadilika,kwa ajili ya tofauti ya personality za watu.

Samia Suluhu akishamaliza kuunda Serikali yake,tutaona vituko, tutaona vioja. Hatutamuona Magufuli katika sera zake.
 
Angalau ametoa ule mkanganyiko, japo ni awamu ya sita lakini ilani inatumika ya awamu ya tano au anaandaa ya awamu yake, niweke sawa kidogo hapo chief.
Ilani haina awamu, kwanza neno awamu halipo kwenye katiba na si neno rasmi, ni watu waliamua kulitumia kutofautisha vipindi vya uongozi. Neno hilo hutumika kielezea idadi ya Ma Rais so SSH ni Rais wa sita kwahiyo awamu yake ni ya sita.
 
Naichukulia awamu ni kama safari ya basi kutoka Dar- Tandahimba!
Ni kama dereva wa basi akipatwa na la kumpata njiani, afu utingo ashike usukani, huwezi iita hiyo kuwa ni safari mpya au nyingine, unless urudi ulikotoka na kuiandaa nyingine!
Kama mnakerwa sana na kuitwa awamu ya tano
Basi tuiite 'awamu ya tano-sita! Maana inatekeleza maono na ilani ya awamu ya tano!
Kwa sasa tofauti ni kama utingo ndie anayeendesha basi letu la safati ileile ya kwenda Tandahimba😂🤣😂!
Mapuvu ni ruksa😂😂😂!
 
Back
Top Bottom