Kilichobakia ndio kinamaliziwa maliziwa.
Wenye nchi wanakwenda kuwa watumwa kwenye nchi yao , amini nawaambieni.
Mkuu 'Statesman',
Nadhani nimekwishakuelewa uliposimama, na haupo mbali sana na mimi.
Fanya hivi: mpe nafasi. Anasema wana mazungumzo, na Bagamoyo, Gesi, Mchuchuma, sijui na wapi kwingine...
Tumdai kwa nguvu zote haya mazungumzo anayofanya atufunulie kilichozungumzwa.
Hii miradi yote anayoikimbiza sasa hivi ndio utajiri wetu hasa, kama hatutaambulia kitu hapa, ndio basi tena, maanake hana habari kabisa na mambo ya wakulima na wafanya kazi. Yeye kajizatiti tuuu kuiuza hii miradi.
Sasa nakuomba, huku kulialia kwetu hakutasaidia kitu chochote kwa sasa, kwa sababu kama ni kuuza atauza tu!
Ni bora auze akijuwa kwamba tunajuwa anatuuza na tutapinga kwa nguvu zote kama haturidhiki; na hatutaishia kulialia tu!
Tudai kwa nguvu zote tuelezwe hayo mazungumzo yanakokwenda.
Sasa angalia, hatujui Dangote kapewa nini hadi katoa hadi gigo la mwisho! Si ni bora tujue? Kwa nini tubaki tunalialia kijumla jumla tu?
Akina Zungu na wenzao, tutawatapisha tu tukishajiridhisha, kama wana njama za kutuuza.