Rais Samia Suluhu Hassan: Serikali kufanya mazungumzo kuendeleza mradi wa bandari ya Bagamoyo

Rais Samia Suluhu Hassan: Serikali kufanya mazungumzo kuendeleza mradi wa bandari ya Bagamoyo

Contract content matters

Mkataba alioufuta Magufuli ulikuwa worse kuliko wakati wa ukoloni.
Mkataba uwe win/win na isiadhiri uendelezaji wa bandari zingine
 
Sijawahi kutilia Shaka hii statement yako. Nina uhakika hivyo ndivyo itakavyokuja kuwa. Nilisoma pdf moja hv ya jamaa nikastuka sana.
Hii ndio wazungu wanasema a nail on the coffin.

Tumekaribisha mnyang'anyi chumbani kabisa.

We are done, completely.

Goodbye mother Tanzania.
 
Ukisoma comments vizuri, utagundua kuwa watu hawataki kabisa kutafakari kwa undani ishu ya hii bandari badala yake wanakubali tu kisa itamkomoa magufuli.
Hi ni ajabu sana hii nchi tuna kazi ngumu sana.
Kama mahakama enzi za mwendazake zilivyowakomoa watu kwa kesi za kubambika
 
Binafsi naona maoni ya watu ni 50/50, coz swali la mkataba mpaka leo limekosa majibu.
Wakati wa jpm yeye hakukataa huu mradi ila alikataa terms zake, na ujue hadi rais anatoka hadharani kusema vile ujue walisha jaribu mazungumzo ya kubadili terms ila yalikwama.
Sasa swali jiulize je mchina atakubali kubadili zile terms kisa tu aliyepo madarakani ni mama?
Huoni hapa Kuna kila dalili za kukubaliwa kwa mkataba uleule?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ipo katika mazungumzo ili kuweza kuendeleza mradi wa bandari ya Bagamoyo. Hayo ameyasema leo Tarehe 26, 06. 2021 wakati wa hotuba yake katika mkutano wa 12 wa baraza la biashara.

Rais Samia amesema pia hiyo itakwenda sambamba na mradi wa Mchumchuma na Linganga kuwa nao mazungumzo yanaendelea ili waone mwekezaji atatoa ngapi na Serikali ngapi ili kuweza kuendeleza mradi huo. Akaongeza kuwa chuma imepanda bei duniani hivyo ni wakatk sahihi wa Tanzania kuchamka.

View attachment 1830564

Pia soma:
Big up Mama Samia.
Positive thinking is what is needed.
 
Mkuu we unaamini kuwa mchina atajenga huo mradi kwa faida ya mtanzania?
Mtazamo wangu, mchina atafanya kama alivyofanya nchini Sri Lanka, Watajenga bandari pamoja na Masharti yote lakn mwisho wa siku kwa sababu GOT tunakopa sana kwenye serikali ya China wataichukua bandari yote.
 
Contract content matters

Mkataba alioufuta Magufuli ulikuwa worse kuliko wakati wa ukoloni.
Mkataba uwe win/win na isiadhiri uendelezaji wa bandari zingine
Swali la.msingi unaamini kabisa China watakubali mkataba ambao Tz watanufaika ikiwa pesa yote wanatoa wao?
 
Kwa jinsi nilivyosikia andiko la mradi wa bandari ni wazo la mamlaka ya bandar(TPA) ila hao wachina na waoman wao ni wa toa fedha tu. Sasa maana yake nini hata serikali inaweza kuamua kujenga yenyewe kwa kutumia mikopo zenye. Riba nafuu pesa ikawekezwa kwa sababu ni mradi wa kiuchumi pesa itarudi maana huo mradi sio bandari tu ila kitakua na eneo la viwanda, makazi, n.k. kwaiyo itakua ni moja ya maeneo bora na ya mfano kwa maendeleo ya uchumi
Screenshot_20210626-135220_1.jpg
 
Hii ndio wazungu wanasema a nail on the coffin.

Tumekaribisha mnyang'anyi chumbani kabisa.

We are done, completely.

Goodbye mother Tanzania.
Nakuelewa sana.

Sasa itakuwa hv:

Tumepigwa kwenye Madini. Hatuna kitu.
Sasa, tunaenda kupigwa kwenye Bahari. Tumepoteza.

Sasa, tusikilizie kwenye ardhi maana ndio pekee iliyobaki. Hii nayo tukipigwa basi ndio mwisho wetu rasmi kama nchi.
 
Mtazamo wangu, mchina atafanya kama alivyofanya nchini Sri Lanka, Watajenga bandari pamoja na Masharti yote lakn mwisho wa siku kwa sababu GOT tunakopa sana kwenye serikali ya China wataichukua bandari yote.
Sasa hiki ndicho tunashindwa kutafakari badala yake tunakalia kukomoana kisiasa kwaajili tu ya kuwafurahisha watu fulani.
Yaani mama anatafuta kupendwa na watu wote yaani anataka watu wote furahi ataachia kila kitu ili kufurahisha watu na hilo ndio litakuwa kaburi letu.
 
Kuufufua kwa terms zipi? nilitegemea aseme kuupitia upya huo mradi ajiridhishe na vipengele vilivyomo coz nae alikuwa sehemu ya serikali iliyopita iliyoukataa huo mradi.
Soma kuelewa usisome kumaliza.

Wamefufua mazungumzo kujadiliana kuhusu mradi.
 
Kama mahakama enzi za mwendazake zilivyowakomoa watu kwa kesi za kubambika
Hayo ni mawazo yako na mbaya zaidi ni nje ya mada, we Kama unafikiri adui wa nchi hii ni JPM basi unamatatizo si bure after all huyo jpm unaye pambana naye tayari yuko mbele za haki huko.

Na Kama unaamini kuwa mahakama zilikuwa zinafanya kazi kwa maelekezo ya jpm basi nasasa pia tuamini kuwa mahakama zinatenda kazi kwa maelekezo ya mama au sio ndio Mana watu wanaachiwa ovyo ovyo kwasababu ya maelekezo kutoka kwake au vipi?

Huu sio muda wa kupambana na Magu huku watu wanaenda kukabidhi ardhi kwa mchina miaka 99.
 
Wakati wa jpm yeye hakukataa huu mradi ila alikataa terms zake, na ujue hadi rais anatoka hadharani kusema vile ujue walisha jaribu mazungumzo ya kubadili terms ila yalikwama.
Sasa swali jiulize je mchina atakubali kubadili zile terms kisa tu aliyepo madarakani ni mama?
Huoni hapa Kuna kila dalili za kukubaliwa kwa mkataba uleule?
Natamani kukwambia "tuwe na imani" ila roho inasita, historia ya viongozi wa CCM kwenye hii mikataba sina hamu nao, na isije kuwa sisi ndio tunaenda kuwabambeleza wachina warudi kwa kigezo cha kurudisha wawekezaji.
 
Contract content matters

Mkataba alioufuta Magufuli ulikuwa worse kuliko wakati wa ukoloni.
Mkataba uwe win/win na isiadhiri uendelezaji wa bandari zingine
Na wasiruhusiwe kuwa na sovereignty of the area... etc etc...
 
Back
Top Bottom