binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
Kuna nchi watu hawakwepi kodi mbona, walau watu walio wengi isipokuwa wachache sana walioshindikana. watu wanaona fahari kulipa kodi.Kweli...
Ndio maana TRA wakiwa around na center flani..kila mtu Nduki.
Kuna mambo ukibembeleza bembeleza hayaendi kamwe!
Kitengo cha elimu kwa mlipa kodi hapo TRA mnakunywa chai tu badala msambae mitaani kutoa hii elimu adimu ya kizalendo, kodi zikiwa rafiki na haki watu watalipa bila msukumo, ni suala la muda mrefu kujenga nchi na kuwaelimisha walipa kodi sambamba na sheria kali za kodi, ukikwepa kodi sahihi uliyopangiwa yakupate tu yakukupata.
Rushwa kwa maafisa pia ni jipu, mtu kakwepa kodi 3M, afisa anamwambia nipe 1M tumalizane, hili jambo lina mzizi mrefu sana. Maafisa wa TRA wana mishahara ya kawaida kabisa, huo ukwasi wa ghafla ghalfa wachunguzwe wanakoutoa, Nchi hii tuwe waadilifu jamani.