Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Zile ni chai za yule mzee na wenzake wanapokaa vijiweni
 
Kwasisi tunaoona kwa kutumia jicho la tatu, chato ni mkoa tayari ni suala la muda tu
Ukikidhi vigezo alisikika raisi. Shida ni vigezo si jambo lingine. Ukishakidhi vigezo kwann usiwe mkoa?
 
Ikiwa mkoa,itasaidia nini?itaongeza kipato kwa wananchi?itaongeza ajira?zaidi itaongeza gharama na watumishi tu,RC,DC,RAC ambao hawazalishi kitu zaidi ya kula mishahara tu,
Bora wangesema tujenge kiwanda,Mi Afrika bwana shida sana.inataka mkoa,mie kijana wa bodaboda itanisaidia kwa lipi?
Mtu mmoja aniambie Mara ya mwisho kusikia USA,au UK imeongeza mkoa au wilaya,au jimbo,lini?
 
Hivi mnaosema chato kumejengwa mabangaloo ya habari mbona siyaoni kupitia TV?
 
Nilikuwa naunga mkono mambo mengi ya Dk. Magufuli lakini hili la kutaka kuifanya Chato kuwa Mkoa siliungi mkono hata kidogo, Chato iendelee kubaki aidha Mkoani Geita au iunganishwe tena na Wilaya ya Biharamulo - Mikoa yenye uhitaji wa kugawanywa ni Morogoro na Tabora sio Chato, na Ziwa Burigi ni sehemu ya Mkoa wa Kagera tangu utawala wa Wajerumani, kusema kwamba Burigi hipo Chato walitaka kulazimisha mambo.
 
Amekufa mmeanza kusema ukweli!
 
Hivi mnaosema chato kumejengwa mabangaloo ya habari mbona siyaoni kupitia TV?
Nani anayesema maneno hayo??

Mimi nimesikia watu wanalalamika kuhusu miradi ya maji Chato kipaumbele, Uwanja wa ndege,Hotel ya nyota 3 ya TANAPA,chuo cha beta,hospitali ya wilaya,hospitali ya rufaa, Mbuga ya wanyama...sasa sijui kama hayo ndo mabangaloo au??
 
Itakua unasikiliza Lisu Redio Fm ila kama umemsikiliza rais, mipango ya chato iko pale pale.
Uko sahihi...kwa mujibu wa Rais Chato itakuwa mkoa ....Kama vigezo havitoshelezi kwa Sasa wataelekezwa namna ya kufanya kukamilisha vigezo hivyo...na tayari vigezo vingi tayari...hospitali ya rufaa inakamilishwa, uwanja wa Ndege inakamilishwa ambao hata Boeing zitatua, vyuo, viwanda, miundo mbinu Yaani barabara tayari ni za lami, hoteli nyita tatu inajengwa...na kadhalika na kadhalika...miaka mitatu ijayo Chato itakuwa mkoa...
 
Kwa kifupi nyie ni wapotoshaji.
 
Naww unaamini kuwa itakuwa hivyo? yale ni maneno ya faraja msibani tu hakuna kingine

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…