Mimi nina mwezi na nusu tangu nichanje full. Naendelea kuvaa barakoa kwani najua chanjo si kinga asilimia 100. Ila ukichukua chanjo ukajumlisha barakoa, distancing , kujisanitize au kunawa unakaribia kabisa kujikinga kwa asilimia 100.
Dunia ina lengo la kuukomesha ugonjwa huu. Katika lengo hilo ndipo zinakuja hatua mbalimbali ikiwemo kutoa fedha ili kuziwezesha nchi masikini ( Afrika) . Hata Ulaya zipo nchi zimewezeshwa kifedha ili kupigana na covid 19.
Wanaoona hizi fedha ni mtego ni wivu wao tu unawasumbua. Mbona hapo awali hawakusema ni mtego au kwavile zilichukuliwa kimyakimya zikawekwa mifukoni mwa miungu yao!
Mama endelea kuupiga mwingi. Unafanya kazi inayoonekana, siyo blabla tulizokuwa tunaimbiwa na wale watesaji.