Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Ngoja nijaribu kukuondolea ujinga. Mashirika ya kimataifa - WB, IMF, WHO, ILO, FAO, nk hutumia takwimu zinazopatikana katika nchi ili ku-grade nchi. Kama utatoa takwimu za uongo, grading yao pia itakuwa ya uongo. Magufuli aliambiwa na IMF kuwa uchumi unakuwa kwa 4.5%, akatakaa, kichaa kikampanda, akagombana na IMF huku akisema uchumi wetu unakuwa kwa 7%. Ingetumika 4.5% nani angesema uko uchumi wa kati? Jielimishe. Usiishie kuwa mpiga kura wa CCM tu. Usitumike.

victor solomon - siyo vibaya na wewe ukijielimisha. Nimesoma ulichoandika.
Aliesema tuko uchumi wa kati ni WB au Magufuli?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Tumetolewa kwenye nuru, tumerudishwa gizani. Hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi....UCHUMI WA KATI TULIOKUWEKO umeporomoka kwa sababu ya JANGA LA UVIKO 19.........

Si serikali yenye kuweza kulaumiwa....

Wala si mh.Rais SSH mwenye kulaumika....

Corona
Corona
Corona

#Siempre JMT🙏
 
Mwenye uchumi wake mnamsimanga kila siku ,kaona isiwe tabu ngoja niondoke nao.
Haya sasa mama amekiri kuwa uchumi ule wa kati umeporomoka?
Je bado kuna shaka na uwezo wa utendaji wa JPM?
Enzi za JPM data zilikuwa zinapikwa.
 
Sanasana vita ya Ukraine. Hata kufanya mapenzi imekuwa ngumu. Jogoo hawiki kwa sababu ya vita ya Ukraine. Bahati nzuri wife naye anaelewa madhara ya vita hii.
Mh.Rais SSH yuko sahihi....UCHUMI WA KATI TULIOKUWEKO umeporomoka kwa sababu ya JANGA LA UVIKO 19.........

Si serikali yenye kuweza kulaumiwa....

Wala si mh.Rais SSH mwenye uwezo wa kulaumika....

Corona
Corona
Corona

#Siempre JMT🙏
 
Na bado vipo vingi tu tutavifahamu mbona ni suala la muda tu
 
Uchumi wa kukopa na misaada mbona hamsemi ukweli au sababu ya chuki zenu kwa JPM endeleeni kuupiga mwingi
 
Uongo una mwisho wake. Yule mkuu wa waongo alipoondoka ghafla 17 March 2021, mambo yote yakawa hadharani. Ni vigumu kuongopa siku zote na usigundulike. Unaweza fanikiwa kwa kipindi kifupi tu. Na ndicho kilichotokea.
Alipoondoka tu JPM Mbolea ilipanda kwa asilimia 100 kutoka elf 54 mpaka 130,000. Mwezi uliofuatia tu petroli ilianza kupanda kwa speed ya mwanga hata kabla ya vita ya Urusi. Inawezekana hata hizi bei tulikua tunadanganywa na yule jamaa
 
Sasa tutakuwa na uhakika gani kama hivi sasa takwimu zilizotolewa na selikali ni za kweli?
we jamaa wacha uonho[emoji1]
Marehemu Magufuli alikuwa dikteta aliyekuwa amekosa werevu.

Magufuli baada ya kuona mambo yanaenda mrama, alizuia hadi watafiti binafsi au taasisi binafsi kufanya utafiti na kutoa takwimu ili akiwadanganya wajinga, waweze kuamini na kusiwepo wa kuhoji.
 
Uchumi wa kukopa na misaada mbona hamsemi ukweli au sababu ya chuki zenu kwa JPM endeleeni kuupiga mwingi
Hatuwezi kuingia uchumi wa kati kwa kukopa na misaada. Kama hawatadhibiti matumizi ya serikali na kuongeza uzalishaji uchumi wa kati ni historia kwa nchi hii
 
Back
Top Bottom