Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

View attachment 2176513

“Tanzania yetu ilikwenda tukafika uchumi wa kati tukarudishwa, kwa uwezo wa Mungu wala si uwezo wa mtu, sasa hivi kazi yetu ni kupambana kurudi tulikokuwa tusije tukarudishwa tukaambiwa hamfai tena kukaa hapa, tupambane turudi kule.

“Na kwa mipango na jinsi ninavyoiendesha Serikali nina imani tutakapofika 2025 kama hatujafika tutakuwa tunakaribia, kwa sababu tunatarajia mwaka ujao tutakwenda kukua kwenye asilimia 5 na pointi, miaka miwili inayokuja tutakwenda kufika kwenye 6.8 tuliyokuwa kabla,” Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo leo Aprili 5, Dodoma katika Mkutano wa Kitaifa wa Maridhiano, Haki na Amani ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Tanzania haijawahi kuwa middle income country toka dunia hii imeumbwa.

Taarifa zilizopo ni kwamba Tanzania ilipanda kutoka lower income country na kuwa lower middle income country wakati wa jiwe. Na haijawahi kushuka

Mama afahamishwe vizuri
 
Magufuli alikuwa punguwani,hata yale magawio ulikuwa ni usanii tu.
tocry.png
 
UN ya wapi? Ya mtaa wa Lumumba maeneo ya Mnazimmoja?
Na zile hotuba za UN za kumsifia ameifikisha nchi uchumi wa kati nao walikuwa wanasema uwongo kwakumwogopa JPM, basi alikuwa jiwe kweli kweli!
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi....UCHUMI WA KATI TULIOKUWEKO umeporomoka kwa sababu ya JANGA LA UVIKO 19.........

Si serikali yenye kuweza kulaumiwa....

Wala si mh.Rais SSH mwenye kulaumika....

Corona
Corona
Corona

#Siempre JMT🙏
Wakati tunaingia kulikuwa hakuna UVIKO19? mkumbuke ni Tanzania tu wakati huo kutokana na sera za JPM uchumi wake uliendelea kukua kwa chanya kinyume na mataifa mengo ya dunia...Haki yake hamwezi kuipokonya...Vitabu vimekwisha andika JPM aliingiza nchi uchumi wa kati
 
Tanzania haijawahi kuwa middle income country toka dunia hii imeumbwa.

Taarifa zilizopo ni kwamba Tanzania ilipanda kutoka lower income country na kuwa lower middle income country wakati wa jiwe. Na haijawahi kushuka

Mama afahamishwe vizuri
Samia anadanganywa wazi wazi, mtanisamehe kama na mtukana... But effect ya kufeli kwake form 4 inaonekana
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi....UCHUMI WA KATI TULIOKUWEKO umeporomoka kwa sababu ya JANGA LA UVIKO 19.........

Si serikali yenye kuweza kulaumiwa....

Wala si mh.Rais SSH mwenye kulaumika....

Corona
Corona
Corona

#Siempre JMT🙏
Thibitisha taarifa yako kwa data na takwimu
 
Sula la JPM ni suala la muda tu kupendwa/kuchukia ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu ila kuogopwa ni lazima kwa kiongozi.

Tutaelewana tu, tunakoenda ni kizuri tunachaana na "Ndiyo, mkuu" .
Umesema kweli hapo juu, Ila kuhusu kuondoka kwenye ndio mkuu hapo umekosea ndio kwanza mizizi inajikita.
Juzi tu Simba imeshinda waziri anasema ni jitihada za raisi
 
Nimejisikia vibaya jana nilikua namtanabahisha rafiki yangu wa Madagascar kwa kujimwambafy kwamba tupo uchumi wa kati akawa ananibishia.
Ila kwa mujibu wa WB bado tupo, hatujatolewa ila haireflect uhalisia tulionao.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mh.Rais SSH yuko sahihi....UCHUMI WA KATI TULIOKUWEKO umeporomoka kwa sababu ya JANGA LA UVIKO 19.........

Si serikali yenye kuweza kulaumiwa....

Wala si mh.Rais SSH mwenye kulaumika....

Corona
Corona
Corona

#Siempre JMT[emoji120]
Ni kweli WB wametuondoa uchumi wa Kati? I doubt
 
Watu wanalalamika kuwa tumetoka na imekuwa siri. Na wengi ni hao hao waliokuwa wanasema sio kweli hatumo humo. Very funny 😀
Mkuu Usishangae sababu unafiki ni sifa mojawapo ya utanzania.
 
Back
Top Bottom