Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Mwenye uchumi wake mnamsimanga kila siku ,kaona isiwe tabu ngoja niondoke nao.
Haya sasa mama amekiri kuwa uchumi ule wa kati umeporomoka?
Je bado kuna shaka na uwezo wa utendaji wa JPM?
Utapeli tu, kila ukifika mwaka uchaguzi wanatutangazia kupanda daraja. They did this 2020. Uchaguzi iliisha tunatangaziwa kushuka daraja. Uhuni. 2024/2025 watatungazia tena.
 
Kuna vitu ni aibu kwako, huwezi peleka data za uongo. Wangepeleka data kwamba Tanzania ni sawa na Marekani kiuchumi wangekubali?
 
IMF wanatumia data zao mkuu hawwchukui za serikali.
 
Umesema kweli hapo juu, Ila kuhusu kuondoka kwenye ndio mkuu hapo umekosea ndio kwanza mizizi inajikita.
Juzi tu Simba imeshinda waziri anasema ni jitihada za raisi
Memento:


Haha Asante saana. "Ndiyo, mkuu" umeona ilipotufikusha ?
 


Hii si kauli yangu , Ni kauli madhubuti ya Rais wa nchi Mh Samia Suluhu akiongea kwenye Mkutano wa TCD , hata hivyo pamoja na kuporomoka huko Mh Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa ccm , chama kilichoshika hatamu ya uongozi kuanzia mwanzo hadi sasa , na ambacho kina mchango wa 100% ya Umasikini wa nchi hii , Ametangaza kwamba hadi kufikia 2025 atakuwa kishairudisha Nchi kwenye Uchumi wa Kati ilimokuwemo kabla .

Mungu ibariki Afrika

 

Halafu world bank wanakuambia Tanzania bado ipo uchumi wa kati, sasa huyu rais ametoa wapi hii kauli yake?
 
Utapeli tu, kila ukifika mwaka uchaguzi wanatutangazia kupanda daraja. They did this 2020. Uchaguzi iliisha tunatangaziwa kushuka daraja. Uhuni. 2024/2025 watatungazia tena.
IMF?
 
Uchumi wa kati, na usio na manufaa yoyote yale kwa Watanzania walio wengi, ni useless.
 
Uongo una mwisho wake. Yule mkuu wa waongo alipoondoka ghafla 17 March 2021, mambo yote yakawa hadharani. Ni vigumu kuongopa siku zote na usigundulike. Unaweza fanikiwa kwa kipindi kifupi tu. Na ndicho kilichotokea.
Jiongeze. Angalia kwenye data za WB. Hatujashushwa. Samia atueleze vizuri. Hatujamuelewa. Maelezo yake yanakwenda kinyume na taarifa za WB hadi leo.
 
Data ya mwaka gani hii?
Mkuu si unaingia tu kwenye web ya WB utaona kila kitu, ukisubiri kuambiwa unaweza kuingizwa chaka. Mm nimeona haatujaondolewa, Ila bado najiuliza uchumi gani wa Kati huu ambao hauna uhalisia?
 
Hii ina maana labda mama hakuelewa hii issue toka mwanzo. Jamani mama asaidiwe. Kauli ya leo inamshushia heshima kwa WB na watu wote wanaoelewa haya mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…