View attachment 2176513
“Tanzania yetu ilikwenda tukafika uchumi wa kati tukarudishwa, kwa uwezo wa Mungu wala si uwezo wa mtu, sasa hivi kazi yetu ni kupambana kurudi tulikokuwa tusije tukarudishwa tukaambiwa hamfai tena kukaa hapa, tupambane turudi kule.
“Na kwa mipango na jinsi ninavyoiendesha Serikali nina imani tutakapofika 2025 kama hatujafika tutakuwa tunakaribia, kwa sababu tunatarajia mwaka ujao tutakwenda kukua kwenye asilimia 5 na pointi, miaka miwili inayokuja tutakwenda kufika kwenye 6.8 tuliyokuwa kabla,” Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema hayo leo Aprili 5, Dodoma katika Mkutano wa Kitaifa wa Maridhiano, Haki na Amani ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.