Rais Samia: Tundu Lissu ni mdogo wangu tu, mimi ni Rais na ni dada yake

Na ndio maana tunawaambia Chadema Diaspora na Watanzania wote kuwa watulie na mambo mazuri yanakuja.

Haina haja ya kutaka "kumlazimisha" Mheshimiwa rais
 
CHADEMA is the most destroyed political institution in Tanzania political history. God gives his hardest battles to his strongest soldiers. We’re strong, they fear us, they won’t fight us in fair ground. Stay strong mzee Freeman Mbowe, they’ve destroyed U indeed. #MboweSioGaidi
 
Lakini nao CCM wasiingilie mambo mazuri yenye manufaa kwa nchi kwa sababu ya kulinda maslahi yao ya kiutawala.
Huwezi jua, pengine Mama analijua hilo na ndio maana akawaambia tangu kipindi kile apewe muda.

Niliwahi kuleta uzi humu kumshauri Mheshimiwa rais Mama Samia Suluhu Hassan kwamba asiuanzishe mchakato huu mpaka atakapopata watu sahihi wa kuusimamia.

Najua ushauri wangu umepokelewa kutokana na usikivu wa Mama.

Tuweni na subra wakuu.
 
Ama kwa hakika haya ni maneno mazuri mno na pia ya muhimu sana kutoka kwa "Comforter in Chief" mwenyewe. Licha ya Rais wetu kuwa ndiye "Commander in Chief" kwa majeshi yetu yote ya ulinzi na usalama hapa nchini, lakini hili la kuleta faraja kwa wananchi wake mbalimbalu wanaopitia katika mitihani migumu ya maisha ni la kutia moyo sana.

Aliyemtangulia yeye hakuwa "emotional" bali "materialist", katika misafara yake alitembea na fedha taslimu, na kuamua kumpa yule amtakaye, na aliamini kuwa akifanya hivyo hapo ndipo ataleta faraja. Alimaua kwa makusudi kuvunja katiba na sheria mbalimbali za nchi ili kutoa faraja kupitia "leeway" alizoziweka kwa baadhi ya wateule wake na makundi lengwa ya kimkakati ili apate kufaidika kisiasa.

Faraja haitolewi kwa ajili ya kupata fadhila, bali hutolewa kwa ajili ya kuonyesha kuguswa na tatizo la mtu ama hali ngumu anayoipitia. Faraja inabeba zaidi hisia kuliko muonekano wa vitu. Ndiyo maana watu husema, "tunahitaji msaada wa hali na mali" na wala siyo "mali na hali", kwa kuwa hali inabeba mguso wa kihisia zaidi.
 
Yaani ukitaka kuthibitisha kuwa watu Ni Misukule.

Kumbe masuala ya TOZO, UFISADI, RUSHWA, UKOSEFU WA AJIRA, siyo TATIZO Kabisa.

Tatizo Ni Mbowe, Lissu, Lema na Heche hawapewi CHAKULA wanavyotaka.

Ukiwapa wao hutasikia kelele.
Sisi tusio na chama wala undugu haki zetu tutazipatia wapi?? Waliokimbia Tanzania wako wengi na wako Marekani Ulaya na nchi nyingine je waanze kushika mabango UN,EU na kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania duniani kote ndio raisi ajue shida iliyopo Tanzania??
 
P
Praise team isije ikawa watu wanapiga fweza kisawasawa !!?? Ohoo !! Natania tu !
 
Ndio uwe mwanasiasa sasa ili ndio uweze kusikilizwa unapodai haki zako.
 
Rais mnyenyekevu,
Rais Mpole,
Rais msikivu
Rais mpenda watu wake wote,
Rais Msikivu
Rais Mtulivu
Rais mchamungu
Rais mahiri
Rais Shupavu
Rais Jasiri

Jizi la kura fullstop.
 
Walituletea Rais kichaa, mbaguzi, mwizi, muuaji, mtekaji muonevu roho mbaya.

Ahsante Mungu
 
60 milioni wanasiasa wote eh kweli bongo kuna kazi haki zinatafutwa kwa mtu mmoja mmoja??
Sasa mtu kama mie nisie mwanasiasa au kuwa na hadhi yeyote ile naweza vp kupata nafasi kama aliyopata Lissu na kueleza malalamiko yangu? Au nikiwa na kesi kama ya Mbowe unafikiri ni nani ataenda kuniombea kwa rais ili niachiwe huru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…