PreGE2025 Rais Samia: Tusi-gwajimanize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje. Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbona kelele zinazo pigwa ni chache kulinganisha na idadi ya watu? Halafu mama kasema, tusioneane aibu....., sasa yeye anajitoaje hapo?
 
Mambo Kadhaa kuhusu Askofu Gwajima

1.Mtu mwenye Misimamo katika Vitu anavyoviamini

2.Mtumishi wa MUNGU kweli kweli asiebagua Watu Kwa sababu ya Itikadi zao za Kidini,kabila Elimu jinsia ukanda,vyama

3.ANA HEKIMA mnoo kwa NEEMA ya MUNGU,ya Kuwafahamu watu,majira ni Kipi kifanyike

4.Anajua majira Ya kuzungumza na Majira ya kunyamaza na Azungumze nini

5.KITU ambacho HANA ni WOGA

6.Ametengeneza Watu Wengi wa Namna Yake

7.Maswali yake Ni ngumu sana kumpatia majibu sahii

8.Ukimtega kwa maswali au Maneno utabaki mdomo wazi ukistaajabu Hekima yake

9.Usiwe mwepesi Kumjibu unaweza jikuta umejibu upumbavu mkubwa mnoo hadi watoto wadogo wakashangaa

10.Kabla hajanena wala kufanya chochote anajua kabisa nini kitatokea hivyo siku zote Haofii matokeo

11.Analipenda Taifa lake kuliko chochote, hupenda kujiita Mr Tanzania 🇹🇿

12. Amefanya Mengi na ameongea mengi,ameshauri mengi ya kuiponya nchi yetu na Kuisaidia

13.Hutokea Hasa Taifa linapokuwa kuwa katika nyakati ngumu

14.HUWEZI kumuonga Kwa Vyeo wala Mali

15.Ametumwa kwaajili ya saa na Majira haya 🇹🇿

16.Hafi leo wala Kesho Mpaka amalize Ajenda ya Kiufalme

17.Ukishindwa Kushindana naye Ungana naye tu hata kwa Unafiki kwa Sababu Huwezi Kumshinda

Kama unampenda Gwajima ongeza walao mambo matatu Mazuri kuhusu Askofu Gwajima na share Kwa wingi
#TANZANIA 🇹🇿 KWANZA mengi Yote Baadae.

C & P
 
Wabunge wote wa CCM wapo kimatumbo yao na ndo maana wengi wao mwisho wao wanakufa vibaya
 
Hakika mwanamke ni mwanamke Tu yaani hata uvumilivu wa kuchuja maneno hakuna?
Tanzania tuna bahati mbaya mno huyu mama hakustahili kuongoza nchi hii
 
Nimehuzunika Sana na kukosa raha Leo tumekua Kama warundi, congo, Zimbabwe, Uganda

Sikuwai kujua one day tutakua kwenye huu mkwamo.
 
Tusi samialize nchi yetu watu wakatekwa/wakapotea/wakateswa/wakauawa/wakadhalilishwa nasisi tukaendelea na kazizetu bila kujali.
 
Hadi sasa Gwajima kashinda 3:1
 
Kwa maana hiyo Gwajima ni Yuda Escariot!? Walikubakiana yeye katoa siri Nje!

Gwajima amewasaliti, walitaka wafanye kimya kimya,yeye kaanika juani! Gwajima ni Yuda Escariot wa ccm ,hahahaha,

Kwetu Sisi Gwajima ni shujaa, anataka usalama wetu, anataka kujua kwanini watu wanaotekwa na hakuna hatua zinazo chukuliwa!? Mpaka atekwe nani NDIO watastuka!?


Nadhani wasio julikana sasa tayari code umepatikana, ikifungua utawajua!
 
Mwenyezi Mungu atuamulie UGOMVI.
 
Gwajima hashindani na dola mkuu.
Kitu akikiingilia Rais tayari ni dola regardless aliingia kama mwenyekiti wa chama. I guarantee you, akiendeleza ligi, hakuna rangi ataacha kuona. Hii ni kwa sababu kila mtu kwenye mamlaka atataka ajichukulie credits/ujiko kumuonesha Rais/mwenyekiti kuwa ali mshughulikia Gwajima.
 
Utekaji kuua watu kuwabambikia watu kesi uonevu wenu vitakosolewa kwenye vikao? Kwani huwa mnafanya matendo haramu ya kishetani kwenye vikao?
 
ccm ya sasa imejaa ibirisi watupu ni ccm ya hovyo haijapata kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…