PreGE2025 Rais Samia: Tusi-gwajimanize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje. Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu

PreGE2025 Rais Samia: Tusi-gwajimanize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje. Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu,

Akiwa anazungumza leo, Rais Samia ameagiza kwamba mchakato wa kuchuja wagombea awamu hii unapaswa kuwa na uangalifu mkubwa ili kuzuia CCM isije kuwa Gwajiminized

"Vikao vinavyoenda kuchuja wagombea wakatendee haki. Anayefaa aambiwe anafaa asiyefaa tuseme huyu ana kasoro moja mbili tatu. Tukipitisha wale ambao wanataka na mie niwemo ndo tunapata wale wanaokwenda huko, chama kinakuwa Gwajiminized"

"Tusi Gwajiminize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje "

Huyu hamtaki tena Gwajima huko Ccm.
 
Yaani Mama anaona gwajima hayuko sahihi?

Haya ni mambo ya ajabu sana yanaendelea ndani ya nchi hii.
Washauri wa mama huenda ni Akina Steve Nyerere au Jerry muro wavuta Bangi kwani kabdri siku zinavyokwenda anazidi kuongea vitu vya ajabu ajabu Aibu kwa Taifa
 
Tumefika pabaya kama Rais ambaye anajinasibu kusimamia Demokrasia akiamrisha kamati za teuzi kupitisha na kutowapitisha baadhi ya wagombea badala ya kuachia wananchi waamue wao wenyewe.


Tanzania hamna Uchaguzi tunapoteza pesa za bure.
 
  • Msamiati mpya
  • Mwenye ufahamu alete maana halisi
Nilitegemea wewe kaka mkubwa mbobevu utufafanulie🥺

Binafsi nime tafsiri kua GWAJIMA hakushinda kura za maoni kawe hivyo akabebwa kugombea Jimbo la kawe na JPM ambae alikua anasema nileteenii GWAJIMA nileteenii GWAJIMA nileteenii GWAJIMA

NB. GWAJIMA HAJAWAI KUSHINDWA ngoja tuuone ukuu wa Mwenyezi Mungu kwenye HILI ni Jambo la mudaa
 
Nyerere alituharibia sana.

Gwajima alisema kweli na kweli haitakiwi ndani ya Ccm. Wao ni kusifu na kuabudu viongozi.

Halafu kwa upumbavu watu wanashangilia.
 
Kwenye Press release ya Gwajima kosa lake ni nini katika yale aliyoyasema? Maskini Mdude, Soka, nilizani Watekaji watakemewa wawàrudishe.😭😭 ndiyo hivyo tena. Mungu wa Miujiza ebu dhihirisha uwepo wako utupe Kitendawili cha hawa Watekwaji.
 
Mkuu jibu kwa hoja , gwajima hayo anayoongea mpaka sasa yupo kwa kofia ya chama gani? Na je achoongea kuhusu watanganyika kutwekwa na kupotezwa ni sahihi ama sio sahihi?
Gentleman,
mimi sio mropokaji kama wale viongoz wa kile chama cha uropokaji.
Mimi sio mtu wa kubuni majibu ya uamuzi wa wananchi wa kawe au kua upande upendao wewe.

mimi ni mtu makini bana.
wana kawe waliamua na wataamua pia hivi karibuni kabla ya November 🐒
 
Back
Top Bottom