peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Katika kurekebisha mfumo wa elimu ninashauri Rais aanze na hili nililolisikia leo ambalo sijaamini ,kuwa kila Halmashauti nchini Tanzania ina wakuu wawili wa idara za elimu ( Elimu msingi na Elimu Sekondari).
Ninashauri ateuliwe mtanzania moja moja mwenye elimu na uzoefu wa kutosha kuisimamia idara moja ya elimu itakayokuwa imeungana elimu msingi na sekondari.
Hii itasaidia mkuu moja wa data kusoma Elimu kuanzia msingi hadi sekondari ambako sasa mkuu mmoja wa idea ya Elimu msingi anampelekea mwenzake wa sekondari Wanafunzi wasiojua kusoma.
Pili itapunguza ukiritimba uliopo sambamba na kupunguza gharama Za kuandika idara mbili zinazofanana ndani ya Halmashauri moja
Mwisho mitaala iliyopo imepitwa na wakati na haiendani na Elimu ya juu ambayo nayo inatakiwa pitiewe upya.
Idara ya Elimu ndani ya Halmashauri iwe na watumishi 8 akiwemo mkuu wa idara, hii itasaidia kuongeza Idadi ya walimu darasani kwani walimu wengi wamejificha maofisini hawafundishi.
Prof Adolf Mkenda, anza na hili.