Ndugu unafananisha majukumu ya afisa elimu mkoa na wilaya.. ?? Deo's yeye ndo mwenye Shule na anatakiwa kuziangalia Kwa ukaribu sana..REO ni just supervisors tu. Ipi idara Hpo iwe kitengo??
MAJUKUMU YA AFISAELIMU WA MKOA
Kuwakilisha Wizara ya Elimu na Utamaduni katika ngazi zote za kielimu katika Mkoa.
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, katika Elimu ya Awali na Msingi, Sekondari, Mafunzo ya ualimu, Elimu ya Watu Wazima na Vituo vya ufundi Stadi.
Kuwa Mshauri Mkuu wa Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu mambo ya Elimu.
Kushughulikia upanuzi wa elimu ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi, Elimu ya Watu Wazima, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Kusimamia maslahi ya walimu.
Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya Darasa la Nne na la Saba, Kidato cha Nne na cha Sita, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ufundi katika Mkoa wake ukishirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania na Wizara ya Elimu na Utamaduni.
Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa Shule na Vyuo.
Kusimamia utekelezaji wa kazi za Maafisaelimu wa Wilaya, waliopo katika Mkoa wake.
Kuratibu na kuchambua Takwimu za Elimu katika Mkoa kwa ajili ya mipango ya Maendeleo katika Ngazi za Wilaya, Mkoa na Taifa.
Kusimamia na kuendesha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza katika Mkoa wake.
Kuratibu na kusimamia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ya Msingi na Sekondari ndani na nje ya Mkoa.
Kuruhusu kukariri kwa wanafunzi shule za msingi hadi darasa la 6 kulingana na taratibu zilizopo.
Kuwa mjumbe wa Bodi za Tume ya Utumishi kwa Walimu katika Mkoa.
Kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wilaya, Vyuo vya Ualimu na shule za Sekondari katika Mkoa wake.
Kuwa Mwakilishi wa Afisa Elimu Kiongozi wa Elimu katika Mikutano ya Bodi inayohusu uendeshaji, mipango ya maendeleo, nidhamu, mapato na matumizi ya fedha za shule za sekondari na vyuo vya ualimu katika Mkoa wake kulingana na kifungu cha 10 cha sera ya Elimu na Mafunzo [1995].
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Mkoa.