Rais Samia: Tutafanya mabadiliko kwenye Elimu. Mkuu wa Idara ya Elimu awe mmoja ndani ya Halmashauri

Kua wawili siyo vibaya, ila input na output yao ipoje?
 
Haiwezekani kuwa na mkuu wa idara mmoja kudili na shule zote za msingi na sekondari kwa wakati mmoja. Idara ya elimu ni idara sensitive Sana, Ni idara iliyosheheni takwimu. Haiwezekan kabisa.

Hitaji Ni maboresho ya mazingira ya shule, stahiki za walimu. Utashangaa idara inaunganishwa lkn mahitaji ya watumishi Ni ile ile,na Hakuna maboresho ya msingi.

Tanzania haina uhaba wa walimu kwa kiwango kinachotakiwa. Kuna tatizo ktk mgawanyo wa walimu Kati ya mijini na vijijini kwenye halmashauri za wilaya. Wimbi la walimu kuhamia mijini Ni kubwa sana. Walimu wamelundikana mijini, wengine wanafundisha hadi vipindi 8 tu kwa wiki yenye vipindi 40.Hawana kazi.

Lkn bado tunatoa matakwimu makubwa makubwa ya upungufu wa walimu. Wakati Hawa waliopo wangegawanywa evenly huko vijijini elimu ingeboreka Sana.
 
Sishauri hili wazo kutekelezwa kwake,kikubwa hapa ni watu kuwajibika,kila siku watu wanalalamika kuhusu ajira lakini hapo hapo hao hao watu wanashauri kuminywa upatikana wa nafasi za ajira
 
Acha wivu fanya kazi
 
Kua wawili siyo vibaya, ila input na output yao ipoje?
Mfano meru Dc. Fuatilia output ya afisaelimu sekondari umeone uwezo mdogo alionao wa kusimamia elimu.

Na mshahara analipwa 3.8 milion plus garri , simu na kulipiwa nyumba ya kuishi , japo analala nyumbani kwake.

Cha kufurahisha na cha kushangaza wakuu wote wa idara ndani yahalmashauri wanalipiwa kodi ya nyumba, maji na umeme japo wanaishi nyumbani kwao au nyumba walizojenga.
 
Sishauri hili wazo kutekelezwa kwake,kikubwa hapa ni watu kuwajibika,kila siku watu wanalalamika kuhusu ajira lakini hapo hapo hao hao watu wanashauri kuminywa upatikana wa nafasi za ajira
1. Mkuu wa idara ya elimu ( ambaye atakuwa afisaelimu msingi na sekondari). Awe na PhD .
2. Afisaelimu taaluma msingi 1
3. Afusaelimu taaluma sekondari 1
4. Afisaelimu vifaa msingi 1
5. Afisaelimu vifaa sekondari 1
6. Afisaelimu elimu ya watu wazima 1
7. Afisaelimu utamaduni 1
8. Afisaelimu ufundi na vielelezo 1

Huu utumike uwe ndio muundo wa idara ya elimu ndani ya Halmashauri nchini Tanzania
 
Baada ya rais jiwe kuindoka Naona akili zimeanza kurudi
 
Hivi kile kitabu cha " Chitemo mimi masikini uvivu wangu nyumbani".. bado kipo... vitabu vya vina nyimbo mpaka za kina diamond
 
Ukiwa na utapiamlo wa akili ukaona kauli kama hizi sijui mara tutafanya mageuzi ya Polisi mara tutafanya mageuzi kwenye elimu mara bandari ya Dar es salaam hivi na kadhalika unaweza kufikiri kuwa Tanzania ina Rais.
 
Hata nafasi ya maafisa Elimu kata haijulikani Wana kazi Gani?
 
Comment nyingi zinaonyesha muundo wa uongizi katika elimu ila sio Sera ya elimu!tatizo letu kwenye elimu liko kwenye Sera,kwa mfano Sera ya lugha ya kufundishia ni kizungumkuti,mtoto anasoma kwa kiswahili miaka 7 halafu gafla lugha inabadilika kwenda kidato cha kwanza.kusema ukweli watoto wanachanganywa sana

Siku tukimpata Rais atakaechukua maamuzi magumu atangaze lugha moja ya kufundishia atalisaidia sana taifa kielimu.lugha ya kufundishia iwe moja either kingereza ama kiswahili tusiogipe!
 
Ndugu miaka 12 iliyopita nilifikia ngazi ya mkurugenzi wa idara wizara ya mambo ya nje kabla sijahamia kwenye international organization.

Nimetoa maoni kama mdau wa governmental operations and administration. Nimeshiriki kwenye public sector reforms nyingi sana so nimezungumza kwa experience.

Kuniambia natetea ugali ni argument ya kitoto ungeweza tu kupinga mawazo yangu.
 
Hao ndoo members wa JF sasa ninao wajua
 
Kichwa cha habari,kinaonesha SAMIA ndio kasema.Kwenye maelezo unatoa maoni yako.uandishi gani huu??
Kiongozi hii nyuzi nimwisoma three times na commentaries wote

Frankly speaking ni wewe tu nimekuelewa

Yaan nilikuwa na mkanganyiko wa kimawazo sana kati ya mtoa kauli na aliejazia sauti kwenye huu wimbo

Aiseh jamaa katuweza kweli tunajadili mawazo na maoni yake badala ya kauli ya mtumishi mkuu wa utumishi Tanzania

Sasa hebu hili tuliache, sasa Kwan Rais alisemaje?
 
Nakubaliana na hoja yako tena Afisa Elimu asimamie masuala ya elimu yote kuanzia chini mpk juu
 
Mama ashughulike kwanza ma maafisa elimu waliohusika kutafuna fedha ya madarasa ya COVID19 endapo akifanya hayo mabadiliko.haraka kutakuwa na teua tengua ambayo inakwenda kuficha ushahidi wa ufisadi uliofanyika
Pesa zimeliwa na kamati za kata wala Afisa Elimu hahusiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…