Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Wewe gari za serikali plate namba STM zimeisha chapu na hizi STN zinaenda mwishoni ndani ya miaka mitatu tu si balaa hili matumizi ni makubwa sana ukijumlisha na wizi ndo balaa
 
Wewe gari za serikali plate namba STM zimeisha chapu na hizi STN zinaenda mwishoni ndani ya miaka mitatu tu si balaa hili matumizi ni makubwa sana ukijumlisha na wizi ndo balaa
Zimeisha au zinanunuliwa nyingine? Mahitaji ya vitendea kazi ni makubwa Kila taasisi.

Mlikuwa mnalalamikia V8,saizi mumeingia kwenye Land Cruiser,hivi nyienataka nini hasa?
 
Hii hesabu ya kuwa ni only 2% ndiyo wanazolipa Kodi nchini, mimi naipinga

Hivi hii VAT ya 18% ya bidhaa zote nchini, Kila raia analipa.

Vile vile Kila muamala ya simu, Kila raia analipa.

Hivi hiyo siyo 100% ya wananchi wote nchini wanalipa Kodi hapa nchini??

Kwa hiyo napinga hiyo "fix" anayotupiga Rais Samia kuwa only 2% ya watu nchini, ndiyo wanaolipa Kodi hapa nchini
 
Tin registered
 
Kama mliwaweka si muwaondoe!
 
Na hao watu ni wanaccm na chawa wake.

Si achukue hatua?
 
Acha kujipa hasira na matusi ya bure. Wezi wanajulikana kama walivyo watekaji na watesaji.
 
Kwa hiyo katoa hitimisho gani baada ya kugundua zinaingia mifukoni mwa watu?

Mwenzie alikuwa akisema mtazitapika, na walikuwa wanazitapika.

Atuambie wangapi mpaka muda huu wako jela kwa uchotwaji wa pesa za wananchi?
 
Acha wivu na uvivu wewe kwa wafanyabiashara pambana na watumishi wa umma hasa wanaokusanya mapato hao ndio tatizo.
 
Hakuna kitu unajua shida ya Tanzania mmesoma lakini vitu mnavyoongea ni toafuti na Elimu zenu Wazambia,Zimbabwe na SA hata Botswana kurekebisha kodi walitumia Tume kama hii pana vitu inatakiwa Mama apingwe kwa hoja sio tunapinga kila kitu na sasa SA wanarekebisha kodi pana Tume ilifanya hivyo baadhi ya mapendekezo wanayafanyia kazi baada ya hapo wanapeleka mapendekezo Bungeni huyu waziri kila kukicha anakuja na Tozo mpya ataweza kufanya mapendekezo yaliyo bora kutoka kwa Watanzania na si wale wabunge wachache.
 
Ni kweli, tunakusanya kingi lakini kinaishia mifukoni kwa watu. Inabidi tukae kama taifa tuangalie hao watu ni wakina nani na hatua gani zichukuliwe ili kudhibiti upotevu huo wa fedha ili ziweze kuwanufaisha wannachi wote kwa maana ya huduma za kimaendeleo.

Lakini tatizo lingine tulilonalo ni kutokuwa na vipaumbele. Sisi ni nchi masikini bado, tusijipe hata matumaini ya uongo. Kwa hivyo, fedha zetu inabidi zielekezwe kwenye mambo ya msingi ya huduma za afya, elimu na miundombinu etc..

Inashangaza serikali kutumia bilioni 34 kujenga MAKUMBUSHO. Inashangaza serikali kutumia fedha nyingi kununua magari mapya, na mambo mengine mengi ambayo ilitakiwa zikajenge mabarabara huko na mambo mengine mengi ya kusaidia wananchi moja kwa moja.

Tuamue sasa, tudhibiti mianya ya upigaji (bila upendeleo) na pia tuweke sawa vipaumbele vyetu ili nchi YOTE iendelee na sio maeneo muhimu tu. Kuna baadhi ya maeneo DSM kuna shida kubwa ya maji. Kuna maeneo mkoa wa Morogoro kuna shida kubwa ya barabara hasa msimu wa mvua. Kuna maeneo kuna zahanati chakavu sana na watumishi wachache. Tusijenge makumbusho, makumbusho tayari yapo, tuelekeze kwenye mambo ya msingi, we are not that rich, show off hazifai.​
 
Mbona haitaji CCM kuwa nayo inazichota kodi zetu bila kificho.
Sasa analalamika kwetu ili tuchukue hatua? Tukisema tuandamane kupinga wizi huo atakuwa tayari kutupokea na kutupongeza? Au atawaagiza wale wenye vikofia vyekundu watuzuie ili tusiwaumbue wateule wake!
Kazi ya rais ni kuchukua hatua si kulalamika kwa wananchi.
 
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara lialia hawalipi kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…