Budapest, Hungary
Miklós Németh waziri mkuu wa Hungary anaikumbuka barua ya kutoka kijijini
Baba akiwa kijijini akimuona katika runinga mara tu mwanaye alipoteuliwa kuwa waziri mkuu, kwa haraka alichukua kalamu na karatasi kumkumbushakuwa majukumu aliyopewa yanakwenda na dhamana kubwa.
View: https://m.youtube.com/watch?v=9NSKIu_JZX0
Kuwa watu wote kijijini alikozaliwa wanataka Miklós Németh awe mtu msema kweli muda wote ili wanakijjiji watembee kifua mbele huku wamenyanyua vichwa vyao kufurahia mmoja wao ameweza kuweka historia na legacy iliyotukuka.
Miklós Németh alichaguliwa kwa bahati na chama tawala dola baada ya mtangulizi wake kuondolewa.
Miklós Németh umri miaka 40 tu, aliingia ofisini akijisikia mpweke kwa kuwa vigogo waliomzunguka wote walikuwa wameteuliwa na kuwekwa katika nafasi zao na mtangulizi wake aliyekuwa ana ushawishi.
Vigogo hao waliomzunguka Miklós Németh mgeni aliyeingia kibahati katika nafasi hiyo ya juu serikalini, walikuwa wanajua Miklós Németh hataweza kubakia madarakani kwa muda mrefu kwani Miklós Németh hakuwa na marafiki makada wa juu katika uongozi wa chama tawala.
Vigogo hao wa chama tawala na serikalini walimpa Miklós Németh jukumu zito kurekebisha mambo halafu wangemuondoa.
Miklós Németh kutokana na kukosa ufahamu wa ndani wa mfumo wa chama dola kongwe akaamua badala ya kushughulikia mfumo huo mkongwe akajikita kwa kufungua nchi kiuchumi .
Miklós Németh akamuita waziri wa fedha kumpatia taarifa ya kibajeti inayoonesha uchumi wa nchi unakwendaje.
Miklós Németh akagundua kuna bajeti kubwa zisizoeleweka zinazokula fedha nyingi kupita miradi, lakini kuna mradi uliopewa jina siri lenye herufi tatu tu.
Kumbe herufi hizo tatu katika bajeti ilikuwa ni siri kuu wasiofahamu wengi hata ndani ya chama dola kubwa.
Miklós Németh akaamua bajeti hiyo ya siri ifutwe na kuondolewa iliyokuwa inakula kiasi kikubwa cha bajeti ya taifa.
Vingunge vigogo walio na nguvu kuliko Miklós Németh wakamuita na kumueleza juhudi hizo mpya alizokuja nazo ni hatari kwa mfumo uliopo.
Vingunge wa chama kongwe na wale wa idara za usalama na ulinzi wakamuambia Miklós Németh, sasa tutakusaidia ufahamu nini kinaendelea hivyo panda lifti katika jengo lile utapatiwa ripoti kamili.
Miklós Németh akisindikizwa na wanausalama wakaingia ktk lifti ya jengo hilo nyeti la taifa, na kushangaa lifti badala ya kwenda juu ilionekana dhahiri inakwenda mwelekeo kwenda ghorofa za chini ya ardhi.
Waziri mkuu Miklós Németh kiongozi wa serikali akajikuta katika wasiwasi mkubwa kwa kutofahamu serikali hii aliyoirithi ina mambo mengi asiyoyajua na yasiyojulikana pia na wengi ndani ya serikali. Na lilomshangaza zaidi hata yeye waziri mkuu pia hakuwa amefahamishwa masuala haya mazito.
Miklós Németh akaingizwa katika chumba chenye ramani nyingi ukutani, mezani kulikuwa na vitabu viwili kimoja katika lugha ya KiRussia na kitabu kingine lugha ya taifa.
Miklós Németh akimsubiri mkuu wa wizara ya ulinzi na usalama akagundua nchi inaongozwa kwa ulaghai mkubwa ambao uinaiingiza nchi katika matatizo endelevu yasiyoweza kubebeka, ni muda tu mambo yatakuwa magumu sana kwa nchi yake.
Miklós Németh akakumbuka barua ndefu aliyoandikiwa na babaye kutokana kijijini kwao kuwa
Ukweli Pekee Ndiyo Utakuinua binafsi kama kiongozi na pia kulinusuru taifa toka uongo uliokuwa jadi ya mfumo wa serikali ya chama dola kongwe . ....