Rais Samia unasubiri nini kufunga Ubalozi Israel?

Rais Samia unasubiri nini kufunga Ubalozi Israel?

Rais Samia rudisha Balozi nyumbani mara moja, na kama wao wanayo wa kwao hapo kwetu timua hii ni sauti ya Watanzania.
Sema sauti yako siyo sauti ya Watanzania, umetumwa uwasemee. Jisemee mwenyewe. Kwani Waisraeli waliouawa wakati Hamas wanavamia siyo watu. Jisemee mwenyewe au familia yako tu, huna mamlaka na kauli za Watanzania.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia rudisha Balozi nyumbani mara moja, na kama wao wanayo wa kwao hapo kwetu timua hii ni sauti ya Watanzania.
Wakifunga wala haitakuwa na impact yoyote...hata hivyo wakikusikia na wafunge tu waondoe msongamano usiokuwa na tija kwenye nchi za wenyewe.
 
Mimi huwa nashindwa kuwaelewa watanzania na watu wote, hivi mlipenda sana Hamas walivyoivamia Israel na kuua raia wake na kuteka wengine? Hamas walikuwa sawa kuivamia Israel na Israel alipaswa kunyoosha mikono juu Hamas aendelee kumpiga na kuua raia wake?

Hamas alikuwa sawa ila Israel hayupo sawa kujilinda na kuhakikisha Hamas hampigi tena?
 
Ngoja kwanza Gaza igawanywe mara mbili maana hamjifunzi. Uchokozi wa Egypt, Syria na Jordan kwa Israel mwaka 1947 na 1967 ndio chanzo Cha yote. Israel iliwapiga na kuongeza maeneo. Wangekaa kwa heshima Leo tusingeukuwa hapa.

Hamas nao wameenda wakarudia kosa la kuvamia Israel. Sasa wamesababisha IDF waigawanye Gaza mara mbili. Kaskazini na Kusini.
 
Mimi huwa nashindwa kuwaelewa watanzania na watu wote, hivi mlipenda sana Hamas walivyoivamia Israel na kuua raia wake na kuteka wengine? Hamas walikuwa sawa kuivamia Israel na Israel alipaswa kunyoosha mikono juu Hamas aendelee kumpiga na kuua raia wake?

Hamas alikuwa sawa ila Israel hayupo sawa kujilinda na kuhakikisha Hamas hampigi tena?

Hii vita imeonesha unafiki wa watu wengi. Nakumbuka mtangazaji mmoja wa Aljazeera alifanya utani siku moja baada ya Hamas kuishambulia Israel, ila Leo nashangaa wanalalamika na kulia.

Nilimuona balozi wa Palestine kwenye umoja wa Mataifa anasoma tamko huku analia na kutetemeka.
 
Kwani walitumwa wakapigane🤔 hata wakipigwa wakafa wote hakuna madhara yoyote tunayopata kama nchi kiherehere cha nini sasa🤔 ugomvi wao hautuhusu hata thumni ya nini kujihusisha nao, ni hao hao wapuuzi walimsaliti mwalimu Nyerere kwenye vita ya kagera baada ya mwalimu kuwaamini na kuwatimua Israel, hiyo vita ni yao watajuana wao wenyewe 🤔 Sauti ya watanzania ya nyokoooooo
Hatutaki kuwa na urafiki na wauaji. Mtoa mada yupo sawa
 
Mimi huwa nashindwa kuwaelewa watanzania na watu wote, hivi mlipenda sana Hamas walivyoivamia Israel na kuua raia wake na kuteka wengine? Hamas walikuwa sawa kuivamia Israel na Israel alipaswa kunyoosha mikono juu Hamas aendelee kumpiga na kuua raia wake?

Hamas alikuwa sawa ila Israel hayupo sawa kujilinda na kuhakikisha Hamas hampigi tena?
Kuua siyo kujilinda
 
Hii vita imeonesha unafiki wa watu wengi. Nakumbuka mtangazaji mmoja wa Aljazeera alifanya utani siku moja baada ya Hamas kuishambulia Israel, ila Leo nashangaa wanalalamika na kulia.

Nilimuona balozi wa Palestine kwenye umoja wa Mataifa anasoma tamko huku analia na kutetemeka.
Mimi kwakuwa alianza Hamas, sina huruma nae, Israel ana haki ya kujilinda na kuhakikisha Hamas hainuki tena kumfanyia ushenzi kama alioufanya October 7. Katika hili wala siwezi kuwa mnafiki.
 
Vita ya Israel na palestina ataiamua Mungu mwenyewe.mwanadamu una masharti mawili tu, kuutakia Yerusalemu amani na kuubariki.hutaki kaa kimya.vinginevyo wewe ni adui wa Mungu.Mwanzo 12:3 na Zaburi 122:6.
 
Kuua siyo kujilinda
Wanakufa raia kwasababu ya ushenzi wa Hamas, Hamas anapigana kwa kujificha nyuma ya raia, anamtumia raia kama ngao. Na hii ni sifa ya kipekee ya magaidi.

Israel kwa kuonesha inamjali raia, ilitoa la wapi raia waelekee. Pengine Israel inamjali mpalestina kuliko Hamas.
 
Tulio wengi tunataka hivo na itakuwa subiri uone...It was a mistaken in the first place kwanini kufungua ubalozi kule.
It was mistake yang'wanoko, Kang'welage noko.
Janjaweed usiku wa juzi wamepukutisha watu zaidi mia 2 na ushee ndani ya usiku mmoja tu na Dunia ipo kimyaaa kwasababu perpetrator sio myahudi ama mkristo.
 
Rais Samia rudisha Balozi nyumbani mara moja, na kama wao wanayo wa kwao hapo kwetu timua hii ni sauti ya Watanzania.

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Astagafilullah
 
Back
Top Bottom