PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sasa ulitaka awaachie mbwa hawa mashoga kuja kuchafua amani? mjinga mkubwa wewe hamia Kenya kwenye democracy, hapa toka leta ujinga shughuli utaiona au baki humu kujificha.
Mtu kaja kusikiliza kesi mnasema kaja kuvunja amani , ila anaeteka na kuua watu wasio na silaha kisa wapinzan , huyo ndo mnamuita mtu mwema
 
Yaani hawa wakenya ndio wametujulisha rasmi kwamba lisu na chadema yake wana ajenda ya siri na Tanzania, shtukeni watanzania,

Hawa wameshaharibu kwao sasa wanataka kuharibu na kwetu, Mungu awalaani aisee
Kati ya Kenya na Tz nan kaharibikiwa , yaan watu 180 hatujui walipo ww unaona sw tu , watekaj unawaona wema na wasikiliza kesi ndo wachochez
 
Akizungumza Leo hii Mei 19, Kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la
2024) katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam. Rais Samia amesema wanaharakati waliodhibitiwa katika nchi walizotoka wasituharibie nchi yetu huku akivisihi vyombo vya sheria kuchukua hatua za haraka kila linapotokea jambo la uvunjifu wa Amani.

"Tusiwe Shamba la Bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka...lakini la pili tumeona mtiririko wa wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku" ~ Rais Samia.




Pia soma
Yule Bibi anatafuta kifo
 
Jaji mkuu wa Kenya Willy Mtungi ndio mojawapo ya watovu wa nidhamu?

Au Waziri wa zamani wa katiba na sheria Martha Karua?

Kweli madaraka ya uraisi yanambadilisha binadamu, nahisi huwa wanajiona wao ni Mungu kabisa.

Unakasirika kwa sababu walikuja kusikiliza kesi!

Daaaa, dunia ina maajabu.
Huyo karua alipeleka umwagaji damu huko kenya 2007
 
Huyo karua alipeleka umwagaji damu huko kenya 2007
Aliupeleka Kenya kuutoa wapi?

Tanzania tayari kuna umwagaji damu, hukuona damu ya Mdude Nyagali ilivyomwagwa nikuwekee picha?

Ataleta umwagaji damu gani tena zaidi ya huo?
 
Akizungumza Leo hii Mei 19, Kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la
2024) katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam. Rais Samia amesema wanaharakati waliodhibitiwa katika nchi walizotoka wasituharibie nchi yetu huku akivisihi vyombo vya sheria kuchukua hatua za haraka kila linapotokea jambo la uvunjifu wa Amani.

"Tusiwe Shamba la Bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka...lakini la pili tumeona mtiririko wa wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku" ~ Rais Samia.




Pia soma

1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners!
 
Kama raisi samia anafahamu somo la historia basi ni makusudi.
Nchi ya tanzania ilipata kusifika sana mpaka kusaidia nchi nyingi ambao waliona nchi zao kuwa uditekta.

Kitendo cha hotuba ya jana raisi samia kusema vyombo vya ulinzi vifanye wanavyotaka kuzuia ni kwamba sasa utachinjwa yoyote.
Na ili naweza kuamini hata ubalozi wa USA umeshaona mbele kutahazalisha wananchi wake.
 
Tanzania ni nchi ya amani na mshikamano. Tumepita katika misukosuko mingi bila kuyumbishwa. Lakini sasa kuna ishara za watu kutoka nje, hasa baadhi ya wanaharakati wa Kenya, kuanza kuleta siasa za mgawanyiko nchini mwetu. Tuwe macho.

Kenya imepitia vurugu, migawanyiko ya kikabila, na siasa kali zisizo na mipaka. Matokeo yake ni taifa lenye uhasama mkubwa wa ndani, mashindano yasiyo ya kistaarabu, na matumizi mabaya ya uhuru wa kujieleza. Hili si jambo la kujifunza, bali la kuepuka.

Kumekuwa na taarifa kwamba baadhi ya wanaharakati kutoka Kenya wamekuwa wakivuka mipaka na kuingia Tanzania, wakijifanya watafiti, waandishi, au wanaharakati wa haki za binadamu, lakini kwa ndani wana ajenda ya kuchochea mijadala ya kisiasa inayogawa watu.

Sheria ya Tanzania iko wazi:
👉 Sheria ya Uhamiaji inakataza mgeni yeyote kujihusisha na shughuli za kisiasa.
👉 Sheria ya Vyama vya Siasa (Na. 5 ya 1992) inazuia raia wa nje kufadhili au kushiriki katika shughuli za kisiasa au kampeni.
👉 Sheria ya Huduma za Habari inazuia upotoshaji kwa kisingizio cha uhuru wa habari.

Tanzania si sehemu ya majaribio ya mitazamo ya kisiasa ya kutoka nje. Hatuwezi kuruhusu "copy-paste" ya vurugu, maandamano ya kulipwa, au misimamo ya kugawa watu kwa misingi ya kikabila au kijamii – ambayo imeitesa Kenya kwa miongo mingi.

Siasa ya Tanzania ina misingi ya maadili, kuheshimu mamlaka halali, na kutetea maslahi ya Taifa kwanza. Wanaotaka kuleta siasa za mitandaoni zenye uchochezi, matusi na kutafuta umaarufu binafsi hawana nafasi.

Tuwe macho na “wanaharakati wa kupandikizwa” – si kila anayejifanya mtetezi wa haki ni mpenda amani. Baadhi wanapandikizwa ili kuharibu ndani kwa ndani. Historia ya Afrika imejaa ushahidi wa njama za kisiasa zilizoanzishwa na wageni.

Hatusemi kila Mkenya ni tatizo. Hapana. Wengi ni marafiki, wafanyabiashara, na watu wa kawaida wanaoishi kwa amani nchini mwetu. Tunazungumzia kundi dogo la wanaharakati wa kisiasa wanaotafuta jukwaa la kueneza ajenda zao.

Tanzania ni nchi ya sheria.
🛑 Wageni wasijihusishe na siasa.
🔍 Tuhoji ajenda za wale wanaoonekana kupita mipaka ya ushawishi wa kawaida.
🤝 Tujenge Taifa letu kwa misingi ya amani, umoja, na uthubutu wetu wa ndani.
 
Akizungumza Leo hii Mei 19, Kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la
2024) katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam. Rais Samia amesema wanaharakati waliodhibitiwa katika nchi walizotoka wasituharibie nchi yetu huku akivisihi vyombo vya sheria kuchukua hatua za haraka kila linapotokea jambo la uvunjifu wa Amani.

"Tusiwe Shamba la Bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka...lakini la pili tumeona mtiririko wa wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku" ~ Rais Samia.




Pia soma
Wanajaribu kutushika MATAKO!!! "'waende wakamchezee KASONGO wao sio sisi"
 
Kuna aneharibu Tanzania zaidi ya Samia na kikundi chake?

Wanalazimisha Lugumi awauzie silaha JWTZ ili wapige madili yao ya fedha wakati Lugumi amewekwa mkononi na former Miss Rwanda ambaye ni Jasusi namba moja wa Kagame.

Saivi JWTZ wananyanyaswa na Rwanda just because wanajua aina zote za silaha tulizonazo na haya yote kwa sababu ya Rais , mtoto wake na kikundi chake kutaka kufaidka kwa mgongo wa fedha za malipakodi masikini wa Tanzania.
 
Kama kawaida ya wale wanaoalikwa kumsikilza rais, kazi yao ilikuwa ni kupiga makofi. Kama kawaida ya mtoa hotuba, aliridhika kwamba amesema mambo ya maana. Kiuhalisia, hotuba ilionesha udhaifu wa ufahamu wa mambo.

Hii ni EAC, Mambo ya protocol tumesaini wenyewe na kukubali mambo ya Common market na movement of labour and services. Ndo sababu ya kuondoa VISA. Leo rais anazuiya wanasheria kuja mahakama za TZ! Anawaita ni wanaharakati! Kwani walikuja kuendesha maanadamano? Inabidi rais akubali uelewa mdogo tunaompa ili aweze kujifunza zaidi. Hii ilikuwa chini ya kiwango.
 
Samahani mkuu...
Umemaanisha rais wa fifa ama wasafi...🤔
Ebu ongeza sauti na tuliokaa huku mwishoni tusikie....🙄
 
Back
Top Bottom