Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Kwanini awatahadharishe wasile hadi wakavimbiwa.

Kwa akili zako Tanzania hii kuna mfanyakazi anapokea mshahara unamtosha hadi kuvimbiwa?
Kumbe unajua vizuri kwamba aliwaambia wasile hadi wakavimbiwa?

Kula hadi kuvimbiwa maana yake ni kula nje ya kile unachostahili.

Wewe kama umetoka bara huko nahau, misemo ama methali za kiswahili utakuwa nazo mbali sana . Sio kosa lako.

Ungekuwa mwenyeji wa ukanda wa Pwani basi vitu vidogo kama hivi ni rahisi kuvielewa.
 
Yani mkuu watu wanageuza maana ndo wanaona wako sawa. Alimaanisha upate kile ambacho unasitahili kulingana na kazi yako lakini si kwa kuiba mali ya umma.
Sasa usichokielewa kamba zingine ni ndefu kupitiliza maana wote hamuwezi kua na kamba zinazofanana na hapo ndio pesa unapopata sasa, au bado haujaelewa ? Wengine kamba zao sio fupi, shtuka
 
Wewe lete mipasho hapa ya kichawa chawa usijue fedha za umma zinatapanywa kwa kauli za kijinga kutoka kwa mtu asiyefikiri kabla ya kunena kama mama yenu.
 
Nilikuwa najua una ujinga kidogo kumbe una ujinga mwingi sana.

Narudia hujui majukumu na madhumuni ya kuanzishwa kwa idara ya usalama wa taifa na TAKUKURU.

Nimekuelekeza nenda kasome sheria hizo utaelewa jambo. Kama sheria imekupiga knockout basi tafuta mjuvi wa sheria akusomee nakukutafsiria.

Mimi ni mdaubwa sheria ndiye ninayekwambia kwamba moja ya majukumu ya msingi ya Tiss ama Takukuru ni pamoja na ku detect vitendo vya wizi ama rushwa dhidi ya serikali.

Hujawahi kusikia taarifa ya Takukuru ikisema kwamba "tumefanikiwa kuokoa bilioni 10 ambazo zingetumika kinyume na matumizi kusudiwa"?

Leo Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru katoa taarifa juu ya fedha walizofanikiwa kuokoa ambazo zingetumika kinyume na matumizi tarajiwa.
 
Sasa kama ni hivyo mbona aliwauliza mbona mnakula mpaka mnavimbewa? maana kama kina kula kwa urefu wa kamba yako hauwezi kula mpaka kuvimbewa,hakuna mshahara wa Serikali ya tanganyika uliwahi kumtoshereza mfanyakazi, wafanyakazi wengi wa Serikali wanaishi kwenye mikopo,hilo la mle lakini msivimbewe bado unaamini lipo kwenye mshahara?
 
Sasa hata wakikaa pembeni ndio Nini watu wameiba pesa za kuweza kununua ndege yakisasa kabisa ya mizigo
 
Aisee kuna watu ni wezi jamani

Ndo mna hawa watu wakishakufa mali zao nazo hufa mna huwezi kuendeleza mali ya dhulma na wengine huishia magonjwa ya ajabu tu wakipoteza pesa mahospitalini

Dhulma ni mbaya sanaa

Mifano hai ipo katika jamii zetu tazameni wenyenu

N. b .Tunaishi umri mdogo sana hapa duniani
 
Watanzania tuliowengi tumepokea kwa mshutuko taarifa ya ongezeko la mara mbili na ushee la gharama za kununua ndege yetu ya mizigo.
-Kitendo hiki ni uhujumu uchumi wa hali ya juu na ni ununuzi wa ndege moja.
-Serikali au wananchi walipa kodi watakuwa wamepigwa kiasi gani mpaka tutakaponunua ndege zote 5 kama manufacturer analeta hadithi za spare parts.
-Tunafahamu kuwa ndege inaponunuliwa huwa na package ya spare parts zinazotumiwa mara kwa mara, Je kwenye mkataba huo spare parts hazikuwekwa au manufacturer anazungumzia raw materials za kujenga ndege?
- Serikali ilitoa taarifa Bungeni ni kwamba ndege zinamilikiwa na TGFA (ndege za Serikali) na Air Tanzania wanakodisha toka TGFA.
-Hii ina maana mchakato wa ununuzi unafanywa TGFA na kushirikiana na Hazina au taasisi zingine za Serikali.
-Rais wetu SSH, sisi watanzania tunaimani na wewe na tunaamini unazo taarifa zote kuhusu wahusika wa mchakato wote wa manunuzi.Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT safisha uozo, badala ya kuusafisha nawe unalilia na kutoa matusi, badala ya kuwaondoa wahusika wote na kuwaweka watanzania wengine.wakati uchunguzi na hatua za kisheria zinafuata.

Ushauri
1.Simamisha kazi wahusika wote kupisha uchunguzi wa wahusika wote
2.Tume ya kuchunguza na kupitia mikataba yote ya manunuzi ya ndege zote
3.Majukumu ya TGFA yawe kuendesha ndege za viongozi,
4.Mkataba wa Ukodishaji ndege (TGFA na ATCL) upitiwe upya, badala ya kuwa na minimum fixed charges za ATCL kulipa TGFA, regardless ndege kuwa hewani au kwenye matengenezo (Preventive or routine maintenance).
5.Serikali ilipe madeni ya ATCL (awali) ili kuweka sawa mizania ya ATCL (mpya), ili iweze kukopesheka,na kupunguziwa gharama za uendeshaji, ambazo mwisho wa Mwaka ATCL mpya inaonekana inapata hasara kutokana na utaratibu huu wa taasisi za Serikali kugombea fito wakati zote zinajengae nyumba moja
 
Usichokitolea jasho hakidumu and so u can't be proud off.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…