Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Leo Rais Samia amekasirishwa sana na hotuba ya wizi wa mali za umma baada ya uwasilishaji wa CAG na TAKUKURU ikabidi aseme pumbavu na kisha kurudi na Kingereza 'stupid'.

Sikuwahi kujua kama ipo siku moja Rais Samia Suluhu Hassan awe na hasira kali kama hizi.

USSR
Kuna wakati alisema

Mijitu mijinga
 
.........kwakweli asiwavumilie kabisa watendaji wanaiingizia hasara serikali, ingawa ni bora zaidi hatua za kuwaondoa zingeambatana na kulipa fidia au kufilisiwa, mama awe jasiri tu hawa watu watamuangusha mbeleni........
 
Naomba kuuliza hivi TAKUKURU na watu wa intelligence hawawezi zuia haya mambo Hadi waache wizi umefanyika?
Kuna wakati huwa najiuliza haya hadi kichwa kinataka kupasuka.

Sasa tuna vyombo vingi vya kufuatilia mienendo yote ya manunuzi lakini utakuta wapo kimya hadi CAG agundue ndo wanajifanya kufuatilia.

Sasa watu kama hawa kazi yao unakuta ni kuwaza mambo ya hovyo tu kupambana na vitu visivyo na athari kwa nchi na kuacha kupigania maslahi ya nchi.
 
Sasa tuna vyombo vingi vya kufuatilia mienendo yote ya manunuzi lakini utakuta wapo kimya hadi CAG agundue ndo wanajifanya kufuatilia.
CAG ndie mkaguzi mkuu hawa wengine hawana idhini ya ukaguzi bila taarifa, elewa kwanza maana ya CAG na TAKUKURU na tofauti zao bila kuelewa huwezi pata jibu la swali lako
 
Kuna watu wameongezeka 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Hii lazima itawaondoa wengi sana.. Ngoja tuone, maana Mh. Rais wetu asipowataja kwa majina, hawataachia nafasi zao hata iweje, mpaka awafukuze yeye mwenyewe.

Saa hz wanapigiana simu, " Mkuu vipi, dah, Mama kawaka vibaya, ila hatoki mtu hadi labda atutaje kwa majina, tubane bane hadi tuone" wezi wengine watasema, "ile ni siasa tu, angetaka kutufukuza si angetaja majina kabisa au ungeona kalamu ya Ikulu tayari imetupiga chini, wala tusijali hatutoi bana"

Mh. Rais wangu hao watu washazoea upigaji, piga chini haraka sana, paaaap, wezi hao wakubwa, hawajali kitu hata nukta.
 
Aliwaruhusu wale kwa urefu wa kamba
Sasa urefu wa kamba maana yake ni kula nje ya unachostahili?

Mbona Watanzania wengi ni weupe kichwani ku reason mambo?

Ukiajiriwa kama muhasibu halmashauri maana yake ule kwa urefu wa kamba yako kwa mshahara huo usitake kula zaidi ya unachostahili. Simple like that.

Hata ule usemi kwamba "Kila mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake" una apply hapa kwasababu kama mbuzi amefungwa kwa kamba fupi atakula majani anayoyafikia tu na yule mwenye kamba ndefu hali kadhalika atakula kingi zaidi.
 
Huyo hata afukuze wote mpaka mumewe hamna mwenye akili atamuelewa.

Kiongozi mkuu wa nchi kusimama hadharani na kuelekeza walio chini yake namna wanapaswa kula (kuiba) ulikuwa udhaifu mkubwa sana kiutendaji na kupitia udhaifu huo nchi itaumia sana.
Wewe ndiyo zero kabisa.

Kwamba Rais kusema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake maana yake wewe ukatafsiri kwamba waibe?

Wewe ukiajiriwa kama mwalimu unatakiwa ule kile unachostahili na uridhike nacho na sio vinginevyo.

Sasa ukiridhika na mshahara wa ualimu wa shule ya msingi na kuacha kutamani wa sekondari si ndiyo umekula kutokana ma urefu wa kamba yako?
 
Sicho alichomaanisha usitetee ujinga,ni sawa na walitunga takrima sio rushwa bali asante
Sasa urefu wa kamba maana yake ni kula nje ya unachostahili?

Mbona Watanzania wengi ni weupe kichwani ku reason mambo?

Ukiajiriwa kama muhasibu halmashauri maana yake ule kwa urefu wa kamba yako kwa mshahara huo usitake kula zaidi ya unachostahili. Simple like that.

Hata ule usemi kwamba "Kila mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake" una apply hapa kwasababu kama mbuzi amefungwa kwa kamba fupi atakula majani anayoyafikia tu na yule mwenye kamba ndefu hali kadhalika atakula kingi zaidi.
 
Kwani kula Kwa urefu wa kamba Yako ni Kuiba? Wewe si una Ajira ndio urefu wako au? Kuiba kwani si ndio kuvuka mipaka?
Yani mkuu watu wanageuza maana ndo wanaona wako sawa. Alimaanisha upate kile ambacho unasitahili kulingana na kazi yako lakini si kwa kuiba mali ya umma.
 
Unaondoa watu kama kina Kabudi, Lukuvi, Kalemani alafu unaweka yake mataktaka?

Mav. i matupu
Wewe hao kwako ndo umewaona watakatifu?

Mbona una akili za sisimizi kiasi hicho?

Hata hao ni wapigaji tu kama walivyo wapigaji wengine tofauti ni namna ya upigaji ndo wanazidiana.
 
Mama inabidi uwe mkali kweli kweli hao wezi kwanza fukuza alafu wape kesi za uhujumu uchumi alafu wafilisi mali zote walizonazo then utaona kama kuna kiongozi wa kwenye public sector ataiba bila kutumia akili kama hivi.
 
Wewe ndiyo zero kabisa.

Kwamba Rais kusema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake maana yake wewe ukatafsiri kwamba waibe?

Wewe ukiajiriwa kama mwalimu unatakiwa ule kile unachostahili na uridhike nacho na sio vinginevyo.

Sasa ukiridhika na mshahara wa ualimu wa shule ya msingi na kuacha kutamani wa sekondari si ndiyo umekula kutokana ma urefu wa kamba yako?
Kwanini awatahadharishe wasile hadi wakavimbiwa.

Kwa akili zako Tanzania hii kuna mfanyakazi anapokea mshahara unamtosha hadi kuvimbiwa?
 
Back
Top Bottom