Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Kuna watu wameongezeka 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Mama afanye kazi tunataka kuona watu wakiondoshwa.
 
Mama alisema wale urefu wa kamba zao.
Amesema kuna watu wameongezeka kwa hio kamba zipo pale pale na wanakula vile vile Ila idadi ya mbuzi imezidi, shida ndio hio watu wamekua wengi wengine wapungue msosi hautoshi au haujamuelewa?

Kuna watu wameongezeka 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo
10% mbaya sana aisee,
 
Kateua watu wengi wenye maGodfather, hakuna atayeweza kumgusa.
Na ndiyo tatizo lilipo. Serikalini kwenyewe wamejaaa watu wengi waliopewa nafasi nyeti kwa kujuana/kwa upendeleo! Halafu anategemea kutatokea maajabu!

Watu wataendelea kupiga tu.
 
Leo Rais Samia amekasirishwa sana na hotuba ya wizi wa mali za umma baada ya uwasilishaji wa CAG na TAKUKURU ikabidi aseme pumbavu na kisha kurudi na Kingereza 'stupid'.

Sikuwahi kujua kama ipo siku moja Rais Samia Suluhu Hassan awe na hasira kali kama hizi.

USSR
Tena ktk katk ya mwezi mtukufu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
........kuna kitu tayari mama atakuwa ameanza kukisoma nakukielewa kuhusu watendaji na viongozi wetu, nina imani kuna hatua kali anaweza kuchukua toka sasa, hawezi kukubali kuvunjiwa heshima na imani kwa wananchi........
 
Dola milion 37 mpaka 86, kama ni chozi lazima limwagike
37 hadi 86 wazee wa 10% wamepeana mgao huo haujaelewa bado na idadi ni kubwa ndio maana pesa imepaa kwa hio anasema watupishe maana wapungue idadi ya walaji kwenye hizo kamba ni kubwa wengine wapungue, sasa nani yupo tayari kupungua hakose vibunda ? Na nani alichora mchoro wa hizo 10% ? Swali linarudi kwa mama
 
Mbona kama mna akili ndogo sana ,hivi kula Kwa urefu wa kamba Yako Kuna shida kwenye hiyo Kauli?

Kwamba Ile methali ya Kila mbuzi hula Kwa urefu wa kamba yake Ina walakini?

Wewe Ukiwa muajikiwa hujui urefu wa kamba Yako? Kuiba si ndio kuvuka kamba? Hapo Kuna tatizo gani mbona mna shida mahala kwenye uwezo wenu wa kufikiri?
Haelewi methali za kiswahili.Kula urefu wa kamba yako,maana yake ale kile kilicho halali kwake,kama vile mshara wake.
 
Kuna jirabmni angu Ni mtumish wa serkalini amejenga nyumba kamaliza Yuko kwenye finishing SAS usipme hzo finishing anazo let's Ni ya gharama ya juu Zaid ,Jana kaleta nyasi kutoka Moshi ,Kisha kaja na maarumaru paving za Chini kafikisha na lorry tatu jamaa walishusha vifaha Hadi asubuhi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
........kuna kitu tayari mama atakuwa ameanza kukisoma nakukielewa kuhusu watendaji na viongozi wetu, nina imani kuna hatua kali anaweza kuchukua toka sasa, hawezi kukubali kuvunjiwa heshima na imani kwa wananchi........
10% ndio mwiba usisahau hilo kitu kimepita 100% kimeenda kudondokea 110% haujaelewa bado au?
 
Back
Top Bottom