Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Hapo ameshatoa maagizo kazi kwa walio Chini yake kuwashugulikia wahusika haiba ya upole inamfanya hata kitu cha umakini kionekane cha kawaida Kwa wananchi na viongozi walio Chini yake. Hiyo pesa imeliwa kwa nyororo ndefu sana Kwa wizara zaidi ya moja lakini watabebeshwa zigo watu tofauti ili kuendelea kulindana Tu. Mchawi wa hii nchi alikuwa fundi haswaaa.
 
Na bado anasema wamepiga 10% hizo ndio asilimia kumi kweli? Mbona wanaleta hasira sana!
Mama kama viatu havimtoshi apite tu hivi asee.
Hujamwelewa. Hajasema wamepiga 10% bali wameongeza ongezeko la 110%.

Maana yake fedha iliyotakiwa kulipwa ni USD 37 million badala yake ikawa USD 86 million.

Sasa hapo kutoka 37 hadi 86 huoni ni ongezeko zaidi ya mara mbili iliyotakiwa kulipwa?
 
Huyu nae kila siku kulialia tu na hakuna hatua za maana anazochukua, kwahiyo hapo anatafuta huruma kwa hao wezi kwamba wajipimie kidogo, au anaamini kwa kulalamika huko ndio wataacha kuiba?

Hapo ni kwenye ndege tu, huko kwingine ni hela ngapi zinavuja? Ujinga kabisa.

Moja kati ya Marais wazembe na incompetent kuwahi kutokea Tz.
 
Mama alipururia kamba kwa muda mrefu. Alifurahi akiambiwa anaupiga mwingi wakati vigogo wanatuibia
Kumbe sasa tunamkumbuka JPM alikuwa sahihi sana aliposema tumekuwa tukiibiwa kwa muda mrefu. Tulimlaumu bure
Too late Mama sasa umebaki unatumia Kiswaenglish kisichoeleweka na wanyonge wa nchi hii. Zungumza Kiswahili cha Makunduchi afadhali
 
CAG ndie mkaguzi mkuu hawa wengine hawana idhini ya ukaguzi bila taarifa, elewa kwanza maana ya CAG na TAKUKURU na tofauti zao bila kuelewa huwezi pata jibu la swali lako
Kwahiyo TISS na TAKUKURU hawana uwezo ama mamlaka ya kuzuia ufisadi ama kuuchunguza na kuchukua hatua?

Acha kuwa layman wewe soma sheria iliyoanzisha PCCB na TISS utaelewa majukumu yao ni yapi.
 
CAG ndio whistle blower anaewaamsha hao wengine kuwapa taarifa wakafanye uchunguzi na hatua zichukuliwe ili kuujua ukweli halisi, I'm not layman like you amka huko usingizini unataka waingilie majukumu yasiyowahusu yaan hakuna taarifa ya rushwa TAKUKURU wakaweke mtego ili kukamata Wala rushwa umerogwa au?
 
Kuna watu wameongezeka 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Aache kulalama watu wanakula Kwa urefu wa kamba zao
 
Unatukana nini Mama...

Pole. Chukua hatua.

Hiyo midege hatuitaki..
 
Back
Top Bottom