Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Kwa hiyo watawaambia hao jamaa wa cancel Invoice au itabidi walipe tu? Nadhani kuna jambo tofauti hapo... Hakuna over Invoice ya namna hiyo. Hata tutusa wa la saba A hawezi fanya ujinga wa hivyo.

Hapo labda wasema walifanya some changes in specifications and customization ya hiyo ndege. Otherwise huyo muhusika kama ni over Invoice wamuweke pale Taifa Kati Watu wajifunzie shabaha tu. Maana hiyo ni stupid kabisa..
Mkataba unamaliza kila kitu.

Hakuna variation ya price namna hiyo mkuu.

To toka 37-87 ?? Ndio maana Rais kakasirika sio Bure
 
Magufuli alidili na hao wezi wakamwita dikteta.

Sasa hivi wamepewa nafasi ya kuiba kelele hakuna wanadai nchi imefunguliwa.
 
View attachment 2570297

Kuna watu wameongeza 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Yaani namba moja wetu amekasirika sana sana.

Lakini tulipokuwa tunapiga kelele kuwa upigaji umezidi na anadanganywa mambo mengi alikuwa anatusoma na kudai sisi watoto wa miaka ya tisini ni walalamishi mno.

Ameshaingia kwenye rekodi ya kuendesha serikali iliyorundika majambazi mengi kwenye utumishi wa umma.

Inabidi na yeye atupishe 2025 maana ameshindwa kusimamia uadilifu serikalini
 
Hadi washtuliwe/watonywe ndio maana kuna majalada we unafikiri wanaenda enda tu kichwa kichwa, wanaambiwa pale ule mradi wa SGR Kadogosa kula pesa anakula anaikung'uta ndio jamaa wanaenda kuchimba, kuchimbua na kuchambua hadi wamnase Kadogosa, unafikiri wanaenda enda tu ?

Unafikiri mtu anaeomba rushwa anakamatwa vipi ? Anavamiwa yaan TAKUKURU wanavamia tu bila taarifa au kutonywa na mtu kua yule jamaa anaomba rushwa ya ngono ? Au wanajua tu wenyewe kua huyu anapokea rushwa ya ngono bila kuambiwa na mtu ? Wanaoteshwa ?
Haya yenye matycoon huwa wananywea maana wanalambishwa mshiko wa maan wanapoteza ushaidi
 
Mkataba unamaliza kila kitu.

Hakuna variation ya price namna hiyo mkuu.

To toka 37-87 ?? Ndio maana Rais kakasirika sio Bure
Bhas hapo tamaa ilizidi weledi wa kazi.

Ni maamuzi ya hovyo. Hata muhusika wa kufanya nae makubaliano hata akikupa hiyo percent bado ataishia kukudharau tu. Hii ni Zaid ya upigaji.. Ni ujinga.. Stupid kabisa
 
siku ile ile tu aliyoleta hii invoice, ningecounter check na jamaa wa Airbus sijui Boeng kuconfirm maana najua hawawezi kufanya huu ujinga lazima kuna dalali kati hapo kufacilitate dili baada yakujilidhisha basi mhusika angekufa kimya kimya na wenzie wote kwenye chain pamoja na kufilisi mali zao.

Mpaka kufika leo CAG analeta hiyo report basi ubwabwa wa matanga watu wangekuwa wameshaula tayari.
 
Back
Top Bottom