Rais Samia: Wananitukana wakitaka niwajibu, sasa siwajibu..
Na mimi kazi mliyonipa nasimama na ninaifanya na mnashuhudia matusi ninayotukanwa mpuuzi, hana maana, huyu Bibi ana hivi, mambo tele lakini najigeuza chura.

Kwahiyo nyingi zinapigwa kelele wakiona haujibu sasa tulitukane litajibu ama halijibu, sijibu nageuza chura masikio sisikii kabisa, ninachotaka mageuzi ya kiuchumi ndani ya nchi hii sitaki kingine sasa kwenye mageuzi haya tutakanyaga nguru wa mshihiri, anayetaka kunikera na mimi anikanyagie uchumi wangu,"
Mama yenu kageuka chura sasa
 
Nakumbuka magufuli aliwahi kusema yeye ni rais jiwe kweli kweli, lile jina la jiwe mpaka leo akiwa amefariki bado halijamtoka!
Sasa huyu wakwetu mpedwa wetu anajinasibu na chura!!!
Kuwa na adabu wewe, unataka kusema ni chura kwelikweli!? Kama umeshindwa kumuheshimu kama Rais wako basi muheshimu kama Bibi/Mama yako. Uhuru wa mtandaoni usitulevye.
 
Na mimi kazi mliyonipa nasimama na ninaifanya na mnashuhudia matusi ninayotukanwa mpuuzi, hana maana, huyu Bibi ana hivi, mambo tele lakini najigeuza chura.

Kwahiyo nyingi zinapigwa kelele wakiona haujibu sasa tulitukane litajibu ama halijibu, sijibu nageuza chura masikio sisikii kabisa, ninachotaka mageuzi ya kiuchumi ndani ya nchi hii sitaki kingine sasa kwenye mageuzi haya tutakanyaga nguru wa mshihiri, anayetaka kunikera na mimi anikanyagie uchumi wangu,"
Na abakie hivyo hivyo Kwa kuwapuuza.Atakuwa anawajibu Kwa matokeo 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/C8ExJKICghn/?igsh=MTViMXNrdGw4eThkeA==
 
Hakuna mtu atamtuka kama anavyojinasibu, ikiwa atasimamia Utawala bora, adhibiti rushwa, ufisadi. Hii awamu watu wanajichotea, hakuna wa kuwauliza. Madawa ya kulevya yamerudi kwa kasi. Mmomonyoko wa maadili n.k
Anyway tumekuelewa Chura...
Hakuna anayechota. Ni mbwembe zenu baada ya kuona hamna cha kuongea tena. Mlihitaji mikutano ya siasa kabla hamjajipanga cha kusema. sasa mmebakiza kuvurumisha matusi tu. Lini akina mdude wakawa wanasiasa. Siasa no sayansi ndugu siyo sheria kama lisu alivyo.
 
Acha tumsifie
IMG-20240610-WA0025.jpg
 
Mnakopa halafu watu wanafanya misappropriation ya mikopo halafu unasema mtalipa wakati mzigo unawaangukia wananchi huku viongozi wakificha pesa ughaibuni?
Kila mtanzania anajionea namna kazi kubwa za kimaendeleo zinavyofayika hapa Nchini. na namna miradi mbalimbali ya kimkakati ilivyokamilika kwa wakati na kuleta matokeo chanya kwa watanzania
 
Ndugu zangu Watanzania,

Leo imekuwa siku ya moto sana na ngumu sana kwa wanasiasa uchwara wa Nchi hii.Leo Rais wetu mpendwa ameshusha NONDO za hatari sana zilizowakosha watanzania na kuibua shangwe kwa watanzania mbalimbali waliokuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka ikulu.

Ambapo Rais Samia amesema ya kuwa amekuwa akitukanwa sana na watu ambao wanataka awajibu lakini amekataa kuwajibu.na badala yake kuendelea kuchapa kazi kwa kasi katika kujenga uchumi wetu.amesema wapo wengine mara wasema mama huyu hafai mara ooo kafanya hivi kafanya vile .lakini anasema yeye hasikilizi Makelele na badala yake anaangalia kazi iliyo mbele yake ya kuujenga uchumi ambao unaendelea kuimarika na kufanya vyema kila iitwayo leo.

Amesema ila yule atakayekwamisha juhudi zake za kuujenga uchumi wetu na mageuzi yake ya uchumi kwa hakika huyo atamkera sana.

Kwa hakika nipo sahihi kabisa naposema kuwa Rais Samia ni Jemedari hodari ,Ni Chuma cha Reli kwelikweli,Jasiri Muongoza Njia ,ni Mama wa shoka ,shujaa wa Afrika na Mwana mageuzi ya kiuchumi. Mungu atupe nini Zaidi ya zawadi hii ya kipekee kabisa ya kutupatia Rais SAMIA ? tunataka nini watanzania wenzangu? Kwanini tunataka tuje kuanza kujuta baadaye na kububujikwa machozi ya majuto ya kumlilia na kwenda kumpigia Magoti Rais Samia arejee tena madarakani?

Tutapata wapi Mwingine aina ya Rais SAMIA?mama mchapa kazi, mama mwenye huruma,upendo,ukarimu, unyenyekevu na mama mwenye kuwajali Watanzania? Kwanini tunataka kumkatisha tamaa mama huyu MZALENDO wakweli na dhati kwa Taifa letu? Kwanini tunataka kuchezea bahati hii tuliyonayo?Hamuoni hata DUNIA itatushangaa na kutuona hatujitambui? Embu tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na kuhakikisha kuwa Tunampeleka na kumrejesha Ikulu kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima hapo Mwakani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Ni kweli kajiita CHURA?
 
Back
Top Bottom